MAGONJWA YA KURITHI NI YAPI?

 KURITHI

• • • • •

MAGONJWA YA KURITHI NI YAPI?


Katika Mgawanyo wa magonjwa,magonjwa yanaweza kugawanywa katika makundi mbali mbali kulingana na muktadha wa mazungumzo husika. Mfano; kama tunazungumzia kuhusu kuambukiza tuna makundi mawili ya magonjwa yaani; 

Magonjwa yakuambukiza kwa kitaalam hujulikana kama Communicable diseases, pamoja na magonjwa yasio ya kuambukiza yaani kwa kitaalam Non-Communicable disease.


Lakini pia katika muktadha wa Vinasaba tunaweza kuwa na Mgawanyo kama huu; Kuna Magonjwa ya Kurithi na ambao sio yakurithi. Na kwa leo tutaongelea orodha ya magonjwa ambayo ni ya kurithi.


ORODHA YA MAGONJWA YA KURITHI NI PAMOJA NA;


1. Ugonjwa wa pumu au Asthma ni miongoni mwa magonjwa ya Kurithi,japo ifahamike kwamba ugonjwa huu ambao hushambulia Mfumo mzima wa Upumuaji umegawanyika pia katika makundi mawili,kuna pumu ya kurithi na kuna pumu ambayo sio ya kurithi


2. Baadhi ya magonjwa ya macho ambayo husababisha upofu,kuna baadhi ya magonjwa yamacho yanayotokana na vimelea vya vinasaba kutoka katika koo yenye tatizo hilo,ambapo kwa asilimia kubwa huleta upofu kwa mtoto kabla ya kufika miaka mitano Mfano; Ugonjwa wa mtoto wa jicho au Congenital Cataract


3. Tatizo la Kuwa Mbilikimo, Pia shida hii huweza kutokana na kuweko kwa vinasaba vya shida hii katika koo Flani,hivo kupelekea vizazi vya koo hiyo kuwa na tatizo hili la Umbilikimo


4. Matatizo ya Kifafa, Japokuwa shida hii pia huweza kusababishwa na matatizo mengine kama kipindi cha Ujauzito(kifafa cha mimba),  au kuwepo kwa mashambulizi ya magonjwa mengine mbali mbali kama vile; Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, N.K. Bado kuna kifafa kinachotokana na urithi wa vinasaba vya tatizo hili katika koo husika.


5. Matatizo ya Akili, Japokuwa si kila mwenye matatizo ya akili basi karithi,ila yapo pia matatizo ya akili mengine ambao huchangiwa na uwepo wa vimelea vya vinasaba vya matatizo hayo katika koo husika.


6. Tatizo la Ualbino, shida ambayo hutokea kutokana na Ngozi kushindwa kupata rangi yake kwa sababu ya upungufu au ukosefu wa Melanin ambayo huhusika na kuipa ngozi rangi yake ya kawaida. Tatizo hili pia huweza kuchangiwa na uwepo wa vimelea vya vinasaba hivi vya Ualbino katika ukoo husika.


7. Ugonjwa wa Sickle Cell au Seli Mundu,Ugonjwa huu huambatana na mgonjwa kuishiwa na damu kila mara na chanzo cha ugonjwa huu huweza kuwa ni kurithi kwa vinasaba kutoka kwa wazi ambao hawakuonesha dalili zozote za ugonjwa huu ila wana vimelea Yaani kwa kitaalam tunasema ni CARRIER wakazaa mtoto. Wazazi hawa huchangia kuzaa mtoto ambaye anashida hii kwa zaidi ya asilimia 25%.


KUMBUKA; Tafiti zinaonyesha kwamba Matatizo mengine kama KISUKARI,AU KANSA hunyemelea koo zile zile ambazo kuna watu wenye shida hizo.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!