MAMA MJAMZITO KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA(POSTTERM PREGNANCY)

MJAMZITO

• • • • • •

MAMA MJAMZITO KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA(POSTTERM PREGNANCY)


Kwa kawaida Ujauzito kuanzia wiki 37 mpaka 42 ndyo mda tunatarajia kwamba mama mjamzito aweze kujifungua,baada ya hapo asipojifungua ni tatizo. Hivo basi endapo mtoto atazaliwa kabla ya wiki 37 huyo tunamuita Premature baby,yaani mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati, Na pia mtoto akizaliwa baada ya wiki 42 huyo ni post-term baby.


Kwa leo tutanzungumzia kuhusu mama mjamzito kupitisha Mda sahihi kwa ajili ya kujifungua pamoja na Sababu zake.


ZIPO SABABU AMBAZO HUCHANGIA MAMA MJAMZITO KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA AMBAZO NI PAMOJA NA;


1. Mama kuwa na tatizo la uzito kupita kiasi au Overweight akiwa Mjamzito


2. Kuwa na Ujauzito ambayo jinsia ya mtoto ni ya kiume pia huweza kuchangia,tafiti zinaonyesha kwamba,wakina mama wengi waliopatwa na shida hii yakuchelewa kujifungua, wengi wao walizaa watoto wa kiume kuliko wakike.


3. Sababu nyingine huweza kuwa ya kimakosa katika kuhesabu tarehe za matarajio kwa ajili ya mama kujifungua au aliyesoma majibu ya  Kipimo cha Ultrasound kukosea.


4. Pia tafiti huonyesha kwa mama ambaye ujauzito wake uliopita alichelewa kujifungua, basi mama huyo yupo kwenye hatari ya kuendelea kupata shida hii hata katika Ujauzito wa sasa.



5. Hitilafu katika utendaji kazi wa Kondo la Nyuma au kwa kitaalam hujulikana kama Placental Dysfunction, huweza pia kuchangia uwepo wa tatizo hili la mama kupitisha Mda sahihi kwa ajili ya Kujifungua.



MADHARA YANAYOWEZA KUMPATA MAMA MJAMZITO BAADA YA KUKAA MDA MREFU PASIPO KUJIFUNGUA



- Uwezekano wa mama huyo kujifungua kwa Njia ya Upasuaji ni Mkubwa, ili kumsaidia yeye lakini pia mtoto aliye tumboni


- Uwezekano wa kuzaa mtoto mkubwa au Big baby kwa kitaalam ni mkubwa pia


- Mtoto kupata matatizo mbali mbali akiwa tumboni, kama ulizi kupungua kutokana na maji ya uzazi kupungua au kula kinyesi akiwa ndani ya tumbo la mama


- Mtoto kufia Tumboni


- N.K


MATIBABU


Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika hospital kwa ajili ya kumsaidia mama huyu,Njia hizo ni pamoja na;


• Kama hana dalili yoyote ya Uchungu, huweza kupewa dawa za kusababisha uchungu ili ajifungue kawaida ikiwezekana.


• Lakini ikishindikana Njia salama kwa mama na Mtoto ni Upasuaji tu.Hivo mama atafanyia upasuaji kwa ajili ya kumtoa mtoto aliyetumboni.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!