HEDHI
• • • • • •
MATATIZO YA HEDHI YANAYOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE ASIPATE MIMBA
Sababu za mwanamke kutokushika mimba ni nyingi sana ikiwemo; matatizo kama ya uvimbe kwenye kizazi,mirija ya uzazi kuziba,mvurugiko wa vichochoe mwilini yaani Hormone Imbalance N.K, Lakini pia
Kama inavyofahamika Wanawake wengi siku hizi wanapimwa hospital hawana tatizo lolote kila kitu kipo sawa lakini Mimba hawashiki. Hii imewapelekea kuwa na Msongo wa mawazo na kushindwa kabsa cha kufanya kutatua shida zao.
Lakini leo nikuambie tu unaweza ukawa huna tatizo lolote na vipimo vipo sawa kabsa lakini mimba usishike vile vile,
Je unafahamu kwamba kutojua tu tarehe za hatari ili ufanye mapenzi na kushika mimba katika mzunguko wako wa Hedhi yaweza kuwa ni tatizo ambalo hata ukinywa dawa gani hupati mimba.
Sayansi inasema kwamba ili mimba itokee lazima yai la mwanamke likutane na mbegu na kurutubishwa ndipo mimba hutokea, Je kama hakuna yai unawezaje kupata mimba?
Tafsri yangu ni kwamba yai lazima litoke siku za hatari ndyo maana zinaitwa siku za hatari(siku ambazo mwanamke huweza kubeba mimba),hivo kufanya mapenzi bila kulenga siku za hatari,ni sawa na kuweka mbegu za kiume kwenye dumu tupu ambalo halina yai hivo hata ukae vipi urutubishaji hauwezi kutokea.
Lakini pia matatizo mbali mbali yanayohusu hedhi yako yanaweza kuwa sababu ya wewe kutokubeba Ujauzito kabsa, ambapo leo ndyo tunazungumzia matatizo haya kwa upande wa hedhi.
MATATIZO YA HEDHI YANAYOWEZA KUSABABISHA MWANAMKE ASIPATE MIMBA NI PAMOJA NA;
1. Tatizo la kubadilika kwa mpangilio mzima wa hedhi kila mara, Mwanamke mwenye Mzunguko wa namna hii hata kupata ujauzito kwake inaweza kuwa shida tofauti na mwanamke mwenye mzunguko ambao haubadiliki badiliki yaani REGULAR MENSTRUAL CYCLE. Mfano kama ni siku 28 basi ni siku 28 period zote.
2. Tatizo la Mwanamke kukaa mda mrefu bila kuona hedhi, Mfano wengine zaidi ya miezi miwili na kuna wengine hata Mwaka na zaidi, wamepima mimba wamechoka kwa kuwa na wasiwasi kwamba labda ni mimba lakini hamna.
3. Kupata hedhi zaidi ya Mara moja ndani ya mwezi mmoja huweza kuwa chanzo cha mwanamke pia kushindwa kubeba mimba
4. Wanawake wengi hupata maumivu ya tumbo wakati wa hedhi,lakini maumivu ambayo mpaka unalazwa hospital sio dalili nzuri,lazima ufanyiwe uchunguzi wa kina huenda una tatizo lingine kama vile; maambukizi katika via vyako vya uzazi.
5. Kupata hedhi ya matone matone tu katika mzunguko wa hedhi, na mara nyingi huwa haina mpangilio maalumu. Shida hii inaweza kukusumbua sana pale utakapohitaji kubeba mimba
6. Mwanamke kublid kupita kiasi na kwa muda mrefu wakati wa hedhi, Mfano; mwanamke anaweza kubadilisha pedi nne na kuendelea kwa siku moja na hali hii ikakaa zaidi ya wiki moja,hilo ni tatizo unahitaji tiba.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!