UPUMUAJI+KIFUA
• • • • • •
MATATIZO YA UPUMUAJI NA KUBANWA KIFUA
Zipo sababu mbalimbali za mtu kupanwa na kifua pamoja na kushindwa kupumua na miongoni mwa sababu hizo huhusisha mashambulizi ya Magonjwa mbali mbali kama vile; Magonjwa ya mapafu, magonjwa ya Moyo, Ugonjwa wa Mafua, Ugonjwa wa corona na magonjwa mengine yote yanayohusisha Mfumo mzima wa Hewa kama vile Asthma(Pumu), Ugonjwa wa Pneumonia,Kansa ya kwenye Koo N.K
Hivo basi katika makala hii tunachambua kuhusu baadhi ya vyanzo vikuu kwa mtu kupata matatizo haya ya Kushindwa kupumua,maumivu ya kifua pamoja na Kubanwa na kifua..
SABABU ZA MATATIZO YA UPUMUAJI NA KUBANWA KIFUA NI PAMOJA NA;
1. Matatizo ya Moyo
2. Shida ya mtu kubanwa na Misuli ya Kifua
3. Mtu kuwa na tatizo la Pumu au Asthma
4. Uwepo wa magonjwa yanayohusu Mapafu
5. Kupatwa na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona
6. Mtu Kuwa na tatizo la Pneumonia
7. Kupatwa na tatizo la Kuvimba kwa Kongosho
8. Kupatwa na matatizo yoyote yanayohusisha Mbavu huweza kuwa chanzo kikubwa cha mtu kushindwa kupumua na kubanwa Kifua
9. Kupatwa na tatizo la kuziba kwa Mishipa ya moyo
10. Mtu mwenye matatizo ya Kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB
11. Mtu kupatwa na Ugonjwa wa Mafua
DALILI ZA KUWA NA MATATIZO YA UPUMUAJI NA KUBANWA KIFUA
• Mtu kuanza kupata maumivu makali ya Kifua wakati wa Kupumua
• Kupata maumivu ya mbavu wakati wa kupumua
• Kuhisi ukosefu wa hewa ya kutosha licha ya kujitahidi kuvuta hewa
• Kupata shida sana ya kupumua
• Mwili kuanza kuishiwa na Nguvu
• Wengine kuanza kubadilika rangi ya Ngozi na kuwa blue,Hii inatokea sana kwa watoto Wadogo
• Kuanza kupata mafua ya mara kwa mara
• Sauti kukauka au kubadilika hasa wakati wa kuongea
MATIBABU YA MATATIZO YA UPUMUAJI NA KUBANWA KIFUA
- Kama nivyoelezea kuhusu vyanzo mbali mbali vya matatizo ya upumuaji na kubanwa kifua, ndivo hivo hivo matibabu yake hujikita katika chanzo husika, Hivo basi,kama Mtu anatatizo la upumuaji au Kubanwa na kifua kwa sababu ya magonjwa ya mapafu au Moyo, na matibabu yake yatahusu magonjwa ya moyo au mapafu N.K
- Endapo unahisi tatizo hili la kubanwa na kifua pamoja na kushindwa kupumua ni vizuri kwenda hospital kwa ajili ya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha tatizo lako ili upate tiba sahihi kwako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!