MTOTO KULIA
• • • • • •
MBINU ZA KUMBEMBELEZA MTOTO ANAYELIA MARA KWA MARA
Endapo umefanya uchunguzi ukajua mtoto wako analia sio kwa sababu ya ugonjwa au matatizo ya kiafya basi unaweza kumnyamazisha kwa haraka na maisha yakaendelea kama kawaida.
Zipo mbinu mbali mbali za kumsaidia mtoto anayelia mara kwa mara, japo kubwa kuliko zote ni kujua anahitaji nini kwa sababu mtoto mdogo hawezi kuongea hata kama kuna kitu anahitaji au hakipo sawa yeye hulia tu.Mfano; mtoto akiwa anahitaji kunyonya atalia,ikiwa mtoto anataka kitu chochote atalia,Na hata pia akiumwa homa,tumbo au ugonjwa wowote atalia, au akiona kitu chochote hakipo sawa atalia pia.
Hivo kuwa mbunifu sana wakujua kwa haraka hitaji la Mtoto wako.
MBINU ZA KUMBEMBELEZA MTOTO NI PAMOJA NA;
1. Kumpa mtoto ziwa au mnyonyeshe wakati analia
2. Mbembeleze mtoto kwa kumuimbia nyimbo mbalimbali za kumfurahisha
3. Mpe vitu vya kuchezea au vichezeshe wewe mwenyewe huku mtoto anaangalia
4. Jaribu kuzunguka na mtoto wakati analia usikae naye Sehemu moja
5. Mbali na kumuimbia, pia jaribu kumuongelesha kama vile anasikia na anaelewa
6. Mtoe mtoto sehemu zenye makelele mengi au Epuka kukaa na mtoto mazingira yenye makelele mengi kama vile ya watu wanaongea sana,Redio,au Mziki mkubwa
7. Muwekee mtoto mziki unaohisi anaupenda baada ya wewe kumchunguza kwa kina, kwa sauti ya kawaida ambayo haiwezi muumiza au mkera
8. Muweke mtoto sehemu ambapo hakuna mwanga Mkali, ili ahisi mazingira kama ya usiku, Hii itamsaidia anyamaze na aweze kulala pia
9. Pia mtoto kuoga hasa na maji ya vuguvugu humsaidia kuwa sawa na kutulia vizuri
10. Sugua vitumbo vya mtoto kama unahisi ana maumivu ya tumbo, hii husaidia kupoozesha maumivu ya tumbo, choo kutoka na gesi pia.
11. Mbembeleze mtoto kwa kumuweka na kumbeba mgongoni au kifuani na kanga yako au kitenge
12. Lakini pia kuna vigari au vibembea vya kubebea watoto kama unacho pia unaweza kukitumia
KUMBUKA; Zipo sababu za mtoto kulia ambazo huashiria dalili za hatari kwa mtoto,hivo ni muhimu kuzijuia pia,Mfano;
kilio cha mtoto kinachoambatana na;
- Mtoto kutokunyonya kabsa
- Joto la mwili kupanda
- Mtoto kutetemeka au kushikwa na dege dege
- Mtoto kubalika rangi ya Ngozi na macho kuwa ya manjano
- N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!