MIWASHO KWENYE NGOZI YA PUMBU (PRURITUS SCROTI)

PUMBU

• • • • • 

MIWASHO KWENYE NGOZI YA PUMBU (PRURITUS SCROTI)


Tatizo hili la miwasho sehemu za siri limekuwa likiwasumbua wanaume wengi hasa katika Ngozi ya pumbu au korodani za mwanaume hadi karibu na eneo la Haja kubwa


Ambapo wengi wao huhisi moja kwa moja kwamba wana Ugonjwa wa Fangasi wa sehemu za siri,hivo kuanza tiba ya Fangasi hao Mara moja. Lakini matokeo yake,tatizo bado linaendelea kuwepo pasipo kupona kabsa licha ya kutumia dawa za Fangasi.


HAYA NI BAADHI YA MASWALI WAGONJWA HAWA HUPENDA KUULIZA WAKIFIKA HOSPITALINI


- Doctor nahisi dalili za fangasi naomba kufaham vipimo vinagarimu shingap?


- Dawa mbora ya Fangasi,ni ipi nitumie?


- Doctor nimekuwa na tatizo la fangasi sehemu za siri hawaponi nifanyeje?


- Doctor ninahisi nina tatizo la fangasi naomba msaada wako


NI SAWA KABSA KWAMBA FANGASI HUWEZA KUSABABISHA HALI HII YA MIWASHO KWENYE NGOZI YA PUMBU AU KORODANI ILA SIO FANGASI PEKE YAKE KUNA SABABU ZINGINE KAMA;


• Kuwa na tatizo la Tezi dume


• Mashambulizi ya bacteria au magonjwa mengine katika damu


• Kuwa na tatizo la Ini


• Kuwa na Magonjwa yanayohusisha Figo


• Kuwepo kwa virusi aina ya HPV-Human pappiloma virusi


- Kuwepo kwa tatizo la maambukizi ya Ukimwi


- Kuwa na tatizo la kisukari


N.K


Hivo basi ni vizuri kuongea na wataalam wa afya kabla ya matumizi ya dawa ili kujua chanzo sahihi cha tatizo lako pamoja na matibabu yake.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!