KUWASHWA UKENI
• • • • • •
SABABU ZA KUWASHWA UKENI
Via vya uzazi vya mwanamke vimekuwa vikishambuliwa na magonjwa mbali mbali kama Maambukizi katika via vya uzazi yaani PID, Fangasi N.K. Baadhi ya magonjwa yakionyesha dalili mapema wakati mengine yakichelewa.
Je Kuwashwa Sehemu za Siri kunatokana na nini?
- Dalili za magonjwa mbali mbali kama Fangasi wa Sehemu za siri(kwa mwanaume na mwanamke)
- Magonjwa ya zinaaa kama kasendwe,kisonono, au chlamydia
- Matumizi ya baadhi ya sabuni zenye makemiko sehemu za siri
- Kuwashwa kutokana na magonjwa ya ngozi
- Kuwashwa kunakosababishwa na allergy ya kitu flani, Mfano nguo za ndani,pedi N.k
- Kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na sababu mbali mbali kama Ujauzito au matumizi ya dawa flani,hivo kupelekea sehemu za siri kushambuliwa haraka na magonjwa kama Fangasi,UTI n.k
Mambo ya kufanya baada ya hali hii ya muwasho kutokea
- Fanya usafi wa kutosha mara tu baada ya kukojoa au tendo la ndoa
- Zingatia swala la kuweka mazingira ya sehem za siri kuwa safi mda wote
- Epuka kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri
- Epuka kuvaa nguo za ndani zinazobana
- Jitahidi kubadilisha nguo ya ndani mara tu baada ya kuitumia mfano baada ya siku moja
- Nenda hosptal kwa ajili ya vipimo na matibabu kama tatizo lipo bado
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!