GAUTI
• • • • • •
TATIZO LA GAUTI,CHANZO CHAKE PAMOJA NA DALILI ZAKE
Tatizo hili la Gauti, ni tatizo ambalo huhusisha joint na viungo mbali mbali vya mwili kama viganja vya mikono na vidole vyake au miguu pamoja na vidole vyake.
CHANZO CHA UGONJWA WA GAUTI
• Ugonjwa huu wa gauti husababishwa na mlindikano na uwepo wa kemikali aina ya URIC ACID kwa kiwango kikubwa mwilini hasa katika joint za viungo mbali mbali kama mikono na miguu
DALILI ZA UGONJWA WA GAUTI NI PAMOJA NA;
1. kuwepo kwa uvimbe au nundu katika maeneo ya joint za viungo mbali mbali kama viganja vya mikono na vidole vyake au miguu pamoja na vidole vyake ambapo mara nyingi uvimbe huu huanzia kidole kikubwa cha mguuni.
2. Mgonjwa kupata maumivu makali sana kwenye maeneo yote yenye nundu au uvimbe huo.
3. Mara nyingine mgonjwa hupata dalili za homa au joto la mwili kupanda.
4. Kushindwa kutembea au kutembea kwa shida.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA GAUTI
✓ Acha kabsa au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe
✓ Epuka uvutaji wa Sigara,kwani nayo huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili
✓ Kama una uzito mkubwa au Uzito kupita kiasi fanya mazoezi pamoja na njia nyingine za kupunguza uzito
✓ Kufanya mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako hasa kwa watu wanaofanya kazi za kukaa Mda mrefu
✓ Epuka kula nyama kupita kiasi,hasa nyama ya Mbuzi,Kondoo na hata ng'ombe pia
✓ Unywaji wa dawa hovio huweza kuleta madhara ikiwemo kusababisha tatizo hili la Gauti
•
Kwa Ushauri zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kupitia namba +255758286584
•
PICHA; HUU NI MGUU WA MTU MWENYE GAUTI KALI
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!