TATIZO LA MTOTO KUKOJOA KITANDANI HUSABABISHWA NA NINI?

KUKOJOA KITANDANI

• • • • • •

TATIZO LA MTOTO KUKOJOA KITANDANI HUSABABISHWA NA NINI?


Ni kweli kwamba wapo watoto wengi ambao hukojoa kitandani na wengine inakuwa tatizo hata wanapofikia umri mkubwa bado huendelea kukojoa kitandani. Tafiti zinaonyesha kwamba shida hii ya kukojoa kitandani huwatokea watoto wa Jinsia ya kiume zaidi kuliko ile ya kike. Lakini hakuna sababu ya moja kwa moja kuhusu utofauti wa tatizo hili na jinsia hizi mbili.


BAADHI YA SABABU AMBAZO HUCHANGIA UWEPO WA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


1. Mtoto kula vitu vya maji maji sana kabla ya kwenda kulala,Mfano kunywa juisi nyingi,maji mengi sana au Chai nyingi huweza kusababisha mtoto kukojoa kitandani wakati amelala.


2. Tafiti zinaonyesha kwamba watoto wanaolala kwa mda mrefu zaidi na wenye usingizi mzito zaidi,wengi wao hupata tatizo hili la kukojoa kitandani.


3. Tatizo la mtoto kushindwa kudhibiti mkojo kutoka pale akiwa amelala, na tatizo hili huchangiwa na sababu mbali mbali ikiwemo maambukizi yanayohusu mfumo wa mkojo kama vile UTI.


4. Udogo wa kibofu ambao huchangiwa na ukuaji hafifu wa kibofu cha mkojo hivo kuleta tatizo la kibofu kushindwa kutunza mkojo mwingi. Matokeo yake endapo mkojo ukizidi tu kidogo,basi hutolewa Nje.


5. Tatizo la ukuaji wa mishipa ndani ya kibofu, Kama mishipa ya mtoto bado haijakuwa kufikia kiwango cha kudhibiti utendaji kazi wa kibofu huweza kusababisha tatizo la mtoto kukoja kitandani pale kibofu kinapojaa.


6. Tatizo la vichocheo mwilini, hapa tunazungumzia kichocheo(hormone) ambacho hujulikana kama ANTIDIURETIC HORMONE(ADH) ambacho kinahusika na kupunguza uzalishaji wa mkojo wakati wa usku pale mtoto akiwa amelala, endapo kuna upungufu wa uzalishaji wa ADH basi huweza kusababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi sana wakati mtoto amelala,hivo kupeleke tatizo ya mtoto kukojoa kitandani.


7. Mtoto kuota usku, zipo aina za ndoto mbali mbali ambazo huweza kusababisha mtoto kukojoa kitandani, ndoto hizo ni kama; Mtoto anaweza kuota anakojoa mahali popote,chooni,nje,kwenye chombo N.K na kupelekea mtoto kukojoa  kweli, au mtoto anaweza kuota ndoto za kutisha ambazo humpelekea hali ya hofu na wasiwasi hata kufikia hatua ya kukojoa kitandani.


8. Ubongo wa mtoto ukiwa bado haujakomaa humpelekea kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo au hata kujisadia mwenyewe mahali popote alipo. Hivo hata wakati wa usku mtoto akiwa amelala pia inakuwa vigumu kudhibiti utokaji wa mkojo.


MATIBABU YA MTOTO KUKOJOA KITANDANI


Tiba ya tatizo la mtoto kukojoa kitandani hutegemea sana na chanzo cha tatizo hilo,mfano kama mtoto anakojoa kitandani kwa sababu ya maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo kama vile UTI, Mtoto huyu huweza kupewa dawa za kutibu  ugonjwa wa UTI na kumsaidia mtoto kupona kabsa na hata kuacha kukojoa kitandani kabsa.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!