TATIZO LA MTOTO KUSUMBUA KULA

 MTOTO KULA

• • • • • •

TATIZO LA MTOTO KUSUMBUA KULA


Kulea mtoto sio jambo rahisi kama baadhi ya watu wanavyodhani bila kujua kwamba kuna changamoto nyingi sana katika malezi, na wengine kuchukua baadhi ya mambo ya kuiga na kuanza kuyafanya kwa watoto wao,bila kujali faida na hasara za wanachokifanya.


 Wakina mama wengi hupata sana changamoto ya malezi hasa katika Uzao wao wa Kwanza.Ukweli ni kwamba hata swala la lishe au ulaji wa mtoto wako laweza kuwa ni changamoto kubwa katika malezi yake.


Wengine wamefikia hatua hadi ya kuwakaba watoto wakati wa kula na kuwachapa fimbo watoto ili wale,kwani watoto wanagoma kabsa kula chakula.


Kumbuka pia, watoto hawafanani hivo hata katika malezi, kuna vitu lazima ujiongeze mwenyewe. Ni vizuri kuomba ushauri na msaada wa kimatibabu kutoka kwa wataalam wa afya pale mtoto anapogoma kula chakula kwani matokeo ya mtoto kugoma kula au kutokula vizuri ni pamoja na mwili kukosa nguvu,kukonda,na kukosa kinga ya kutosha kuhimili magonjwa mbali mbali.


SABABU ZA MTOTO KUGOMA KULA CHAKULA NI PAMOJA NA;


1. Kupewa chakula cha aina moja kila siku,hii huchangia hali ya mtoto kukichoka haraka chakula hicho na kuamua kugoma kula


2. Mtoto kula vitu vidogo vidogo mara kwa mara humfanya mtoto ashibe na hata ikifika mda wa kula tayari mtoto kashiba hataki tena chakula.


3. Sababu nyingine ni mtoto kuumwa magonjwa yote yanayohusu tumbo


4. Tumbo la mtoto kujaa gesi hivo kupelekea hali ya kuhangaika,kulia na kutokutaka kula chakula chochote


5. Mtoto kuwa na tatizo la Minyoo,ni miongoni mwa visababishi vikubwa vya mtoto kugoma kula chakula


6. Mtoto akiwa na shida ya Homa au joto la mwili kupanda hata appetite ya chakula hupotea kabsa,hivo mtoto kugoma kula chakula chochote


MATIBABU YA TATIZO LA MTOTO KUSUMBUA KULA


- Matibabu ya tatizo la mtoto kusumbua kula hutegemea na sababu inayomfanya mtoto kukataa chakula,hivo basi lazima mtoto achunguzwe kwa kina kujua sababu ua mtoto kukataa chakula,ndipo matibabu kuanza,Mfano kama mtoto ana shida ya Minyoo; Basi matibabu yatahusu kupewa dawa za minyoo kama vile; Albendazole,mebendazole N.K


MADHARA YA MTOTO KUGOMA KULA CHAKULA NI PAMOJA NA;


• Mwili kukosa nguvu


• Mwili kuwa dhoofu na kukonda


• Mtoto kushambuliwa na magonjwa kwa urahisi kutokana na kinga ya mwili kuwa chini


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!