UGONJWA WA FIGO CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE,MATIBABU YAKE NA WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA
UGONJWA WA FIGO
••••••••••
UGONJWA WA FIGO CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE,MATIBABU YAKE NA WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA
Ugonjwa huu huhusisha Figo, na kusababisha Figo zishindwe kufanya kazi yake kama kawaida, Sababu za mtu kuwa na matatizo ya Figo ni pamoja na;
✓ Kuwa na tatizo la shinikizo la Damu au kwa kitaalam Presha
✓ Kupatwa na maambukizi mbali mbali kwenye Figo,Mfano ya Bacteria aitwaye Streptococci
✓ Kuwa na tatizo la Kisukari pia huweza kuchangia kuleta shida kwenye Figo
✓ Pia kuna magonjwa yanayotokana na Vinasaba katika koo au magonjwa kutokana na kurithi ambayo huathiri Figo
✓ Kutumia Dawa mbali mbali na kwa mda mrefu za kutuliza maumivu Mfano wa Ibrufen
✓ Unywaji wa Pombe kupindukia
✓ Pia Wagonjwa wenye ugonjwa wa UKIMWI wapo kwenye hatari ya kupata matatizo Ya Figo
✓ Kuwa na shida ya Mawe kwenye Figo au kwa kitaalam Kidney Stones
✓ Pia uwepo wa tatizo la Tezi Dume huweza kusababisha matatizo ya Figo
DALILI ZA UGONJWA WA FIGO
• Kuingiwa na shida ya kukosa hamu ya kufanya Tendo la Ndoa
• Mgonjwa kupatwa na shida ya Kuvimba Sehemu mbali mbali za mwili wake Kama Uso, miguu N.k
• Kupatwa na shida ya kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa Usku
• Kupatwa na tatizo la mwili kuwasha mara kwa mara
• Kujisaidia haja ndogo(mkojo) iliyochanyika na Damu
• kupata homa za mara kwa mara
• Mwili wote kuchoka sana
• Kupatwa na tatizo la maumivu chini kidogo ya kitovu
WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA FIGO
- Watu wenye ugonjwa wa UKIMWI
- Watu wenye matatizo mengine kama Presha
- Watu wenye ugonjwa wa kisukari
- Watu wanaokunywa pombe kupita kiasi
- Watu wanaopenda kunywa dawa kali mara kwa mara
- Watu ambao hawanywi maji ya kutosha
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!