UGONJWA WA FIGO NA KUVIMBA MIGUU

UGONJWA WA FIGO NA KUVIMBA MIGUU

• • • • • •


Kwa mtu mwenye matatizo ya Figo huvimba sana miguu na wengine huvimba kwenye macho, Na hii ni kutokana na Kuwepo kwa mkusanyiko wa Sodium na maji pasipo kutolewa Nje vizuri, hivo kupelekea hali hii ya Uvimbe.


.


Matatizo ya Figo hasa katika mishipa yake ya damu kutokufanya kazi , huweza kusababisha ukosefu wa Protein katika Damu na vile vile kuleta matokeo mabaya kama maji kukusanyika hali hii kwa kitaalam huitwa NEPHROTIC SYNDROME.


.


Sababu zingine ambazo huweza kuchangia uvimbe katika maeneo ya mwili kama Miguu ni pamoja na;


- Kupata lishe duni ambayo husababisha Ukosefu Mkubwa wa Protein mwilini


- Kufanya kazi za kukaaa kwa Mda mrefu


- Kusafiri umbali mrefu ukiwa umekaaa


- Matatizo yanayotokea katika Mfumo mzima wa Lyph hadi kusababisha kuvimba



MATIBABU


- Uvimbe wa kawaida wa Miguu huisha kwa kufanya mazoezi ikiwemo ya kutembea, endapo uvimbe utaendelea kuwepo hata baada ya kufanya mazoezi,huwenda kuna shida nyingine kama Damu kuganda hivo nenda hosptal.


- Zipo dawa mbali mbali kwa ajili ya kuondoa mkusanyiko wa Maji mwilini na kuondoa hali ya Uvimbe Kama vile; Lasix au furosemide.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!