DAMU
• • • • •
UGONJWA WA KUHARA DAMU
Tatizo hili linawapata watu wengi hivi sasa na chanzo kikubwa cha Ugonjwa huu wa kuhara damu huhisishwa sana na matatizo ya Ini. Endapo ini limepata shida, moja ya dalili kubwa ni mtu kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na Damu.
HIVO BASI CHANZO CHA TATIZO LA KUHARA DAMU NI PAMOJA NA;
1. Kuwa na matatizo au Magonjwa yanayohusisha Ini
2. Mchafuko wa tumbo ambapo hutokana na sababu mbali mbali,kama kula baadhi ya vyakula vyenye Sumu N.K
3. Uwepo wa maambukizi ya Minyoo
4. Tatizo la kushambuliwa na vimelea vya magonjwa, Protozoa au bacteria mbali mbali
5. Kutumia kemikali au Sumu pasipo kujua
6. Mashambulizi ya virusi mbali mbali Mfano Kirusi cha Hepatitis B Virus ambacho husababisha Ugonjwa wa Homa ya Ini
7. Kuwa na tatizo la Vidonda vya Tumbo Kutokana na mashambulizi ya H.pylori
8. Tatizo la kuvimba utumbo mkubwa yaani COLITIS kwa kitaalam
9. Kuwa na tatizo la Kansa ya Utumbo mkubwa au kansa ya njia ya haja kubwa kwa kitaam huitwa Rectal cancer
10. Matatizo ya bawasiri ambayo huleta hali ya mishipa ya Njia ya haja kubwa kuvimba,kuwa na michubuko pamoja na kuvuja damu
DALILI ZA UGONJWA WA KUHARA DAMU NI PAMOJA NA;
• Kujisaidia kinyesi ambacho ni cha maji maji(kuharisha) ambacho kimechanganyika na damu
• Kujisaidia kinyesi mithili ya makamasi
• Kupata maumivu ya tumbo au njia ya haja kubwa wakati wa kujisaidia
MATIBABU YA UGONJWA WA KUHARA
- Matibabu ya Ugonjwa wa kuhara hutegemea sana chanzo cha ugonjwa huu,hivo nimuhimu kwenda hospital na kufanya vipimo kwanza,ili kujua chanzo cha ugonjwa na kuanza tiba mapema.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!