MWILI KUVIMBA
• • • • • •
UGONJWA WA KUVIMBA MWILI(TAMBAZI)
Ugonjwa huu huhusisha kuvimba maeneo mbali mbali ya mwili wa binadamu kama vile, mapafu,Miguu,tumbo,uso au mikono. Na tatizo hili hutokea endapo maji kutoka katika mishipa midogo midogo ndani ya mwili kutoka na kujikusanya sehemu ya nje au Katika seli hai za mwili.
.
Uharaka wa matibabu pia hutegemea sana na eneo ambalo limeathiriwa na tatizo hili la kuvimba maeneo mbali mbali ya mwili wa Binadamu, Mfano; kama uvimbe huu huhusisha mapafu,ni dhahiri kwamba ni hatari zaidi kwani mgonjwa atakosa hewa pamoja na kupata shida ya kupumua.
WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;
1. Wenye matatizo ya Figo
2. Wenye Ugonjwa wa shinikizo la Damu
3. Wenye magonjwa yote yanayohusisha moyo
4. Wenye matatizo ya Ini
5. Wenye matatizo yanayohusu mishipa kuziba au kuvimba
6. Wanaokunywa Pombe sana
7. Wenye magonjwa ya kisukari
8. Wanaotumia dawa mbali mbali kama zile zinazohusu urekebishaji wa vichocheo mwilini
9. Wanawake wajawazito
10. Wale wanaotumia kiwango kikubwa cha chumvi kwenye chakula
11. Waopenda kukaaa kwa Mda mrefu pasipo kutembea au kufanya mazoezi yoyote
KUMBUKA;
Kama uvimbe upo kwa muda mrefu hata baada ya kufanya mazoezi mbali mbali,Nenda hosptal kwa ajili ya uchunguzi wa kina na kuanza tiba.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMUAU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!