UGONJWA WA PARKINSON NI NINI? DALILI ZAKE NA TIBA YAKE

 UGONJWA WA PARKINSON

••••••

UGONJWA WA PARKINSON NI NINI? DALILI ZAKE NA TIBA YAKE


Huu ni ugonjwa ambao huhusisha ubongo wa binadamu kushindwa kufanya kazi vizuri kutokana na ukosefu wa vichocheo aina ya Dopamini.


DALILI ZA UGONJWA WA PARKINSON


Je mtu mwenye Ugonjwa wa Parkinson utamjuaje?. Dalili kubwa za Ugonjwa wa Parkinson ni pamoja na;



1. Kuwa na hali ya kutetemeka Mikono


2. Kazi za ubongo kuathiriwa kama uwezo wa kutunza kumbu kumbu kupotea


3. Uwezo wa kufikiria kuathirika


4. Mgonjwa kupata shida ya kushindwa kutembea


5. Mgonjwa kujaa hofu na wasiwasi kwa muda mwingi


6. Mgonjwa kuwa na hali ya huzuni kwa kiasi kikubwa katika maisha yake


7. Mgonjwa kupata tatizo la kukosa Usingizi


8. Mgonjwa kuwa hali ya mahangaiko au kutokutulia kila mara


WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


✓ Walio katika ukoo ambao kuna mtu mwenye shida hii,kwani huaminika kwamba vinasaba vya ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine.


✓ Wanaofanya kazi ambazo huhusisha kwa kiasi kikubwa upuliziaji wa makemikali katika mimea.


✓ Ugonjwa huu wa Parkinson hupata Wanaume zaidi ya Wanawake.



MATIBABU


Hakuna Matibabu ya moja kwa moja ya ugonjwa wa Parkinson  mpaka sasa.Ila kuna matibabu yakudhibiti Dalili za Ugonjwa huu kama vile;  


Matumizi ya Dawa kama Sinemet pamoja na Levodopa ambazo huhusika na kuzuia hali ya kutetemeka kwa mgonjwa,hofu,wasiwasi, pamoja na shida ya kushindwa kulala.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!