UTI KWA MJAMZITO
• • • • • •
UGONJWA WA UTI KWA MAMA MJAMZITO
Kwanza ifahamike kwamba hali ya kuwa Mjamzito tayari ni kisababishi Mojawapo cha kinga ya mwili kushuka. Hivo basi mama Mjamzito yupo katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama UTI na FANGASI UKENI kwa sababu ya kushuka kwa Kinga ya mwili kipindi cha Ujauzito hivo kupelekea mama huyu kuwa na maambukizi ya mara kwa mara hasa ya magonjwa kama PID,UTI na FANGASI SEHEMU ZA SIRI.
Pia mabadiliko ya vichocheo mwilini yanayotokea kipindi mwanamke akiwa Mjamzito husababisha mabadiliko mbali mbali katika mfumo mzima wa mkojo ikiwemo mgandamizo mkubwa wa kizazi kushuka chini wakati mtoto anakua hivo kupelekea njia ya Mkojo kubanwa pamoja na kibofu cha mkojo, hivo mama mjamzito kukojoa mara kwa mara, lakini pia kuwa katika hatari ya kupata UTI.
kwa maelezo hayo nafikiri nitakuwa nimeshawajibu wale wanaonifata inbox na kuuliza sana swali hili,kwamba kwanini Mjamzito hupatwa sana na UTI na FANGASI mara kwa mara?
DALILI ZA UGONJWA WA UTI NI PAMOJA NA;
1. Joto la mwili kupanda au Kupata homa
2. Kukojoa mara kwa mara(isipokuwa kwa mama mjamzito)
3. Mkojo kuchoma wakati wa kukojoa
4. Mkojo kutoa harufu kali pamoja na kubadi
lika rangi
5. Kupata maumivu ya tumbo chini kidogo ya kitovu hasa hasa kwa upande wa kushoto
6. kupata maumivu ya joint,misuli pamoja na viungo mbali mbali vya mwili
7. Uchovu wa mwili kupita kiasi
8. Kupoteza kabsa hamu ya kula chakula
9. Kupatwa na maumivu ya mgongo mara kwa mara
10. Kupata maumivu ya kiuno hasa wakati wa kuinama
11. Pia UTI huweza kusababisha hali ya ukavu wa uke kwa mwanamke
MATIBABU YA UGONJWA WA UTI KWA MAMA MJAMZITO
✓ Kutokana na hali ya Ujauzito matumizi ya baadhi ya dawa huweza kuwa hatari na kuleta athari kubwa kwa mtoto tumboni pamoja na mama mwenyewe. Hivo basi hata katika matibabu ya UTI Kwa mama mjamzito baadhi ya dawa za UTI haziruhusiwi.
✓ Dawa sahihi kwa ajili ya matibabu ya UTI kwa mama mjamzito ni pamoja na AMOXCYCLIN
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +25578286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!