VITU AMBAVYO UNAWEZA KUFANYA UKIWA NYUMBANI KUONDOA HALI YA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA KWA MJAMZITO
KICHEFUCHEFU KWA MJAMZITO
• • • • • •
VITU AMBAVYO UNAWEZA KUFANYA UKIWA NYUMBANI KUONDOA HALI YA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA KWA MJAMZITO
Kutokana na mabadiliko ya vichocheo ambayo hutokea kipindi cha Ujauzito, Mama mjamzito huweza kuona mabadiliko mbali mbali katika mwili wake kama Vile; kupatwa na hali ya kiungulia(heartburn), kupata choo kigumu, kuchukia baadhi ya vyakula au harufu,hali ya kichefu chefu na kutapika.
Hali hii ya kichefuchefu na kutapika mara nyingi huanza kutokea wakati wa asubuhi, huku wengine wakitapika mpaka kufikia hatua ya kulazwa hospitalini.
VITU AMBAVYO UNAWEZA KUFANYA UKIWA NYUMBANI KUONDOA HALI YA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA KWA MJAMZITO
✓ Ukipatwa na hali hii ya kichefuchefu na kutapika pendelea Kula tangawizi mbichi au vitu vyenye tangawizi ndani yake kama vile; pipi zenye tangawizi,Biskuti zenye tangawizi, au Chai yenye tangawizi ndani yake.
✓ Usiweke sukari nyingi,chumvi au mafuta mengi kwenye chakula chako
✓ Pendelea kula vyakula vyenye virutubisho jamii ya Protein kama vile, Maziwa, Samaki,Nyama,nafaka au karanga
✓ Jitahidi kupata maji ya kunywa ya kutosha kwa siku
✓ Pia mazoezi husaidia kuondoa hali hii kama unafanya mazoezi ya mara kwa mara
✓ Epuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja bali kula kidogo kidgo alafu mara kwa mara
✓ Pendelea kula vyakula vikavu hasa wakati wa asubuhi baada ya kuamka, Mfano; unaweza kula Mkate ambao ni mkavu pamoja na maji yenye uvuguvugu.
Hii itakusaidia sanaa kama unapata hali hii ya kichefuchefu na kutapika wakati wa Ujauzito.
KUMBUKA; Kama hali ni mbaya zaidi nenda hospital kwa ajili ya kukutana na wataalam wa afya, na kwa ajili ya matibabu zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!