UZAZI
• • • • • •
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUPANGA UZAZI
Kuna mambo mengi unatakiwa kuyafaham na kuzingatia katika swala zima la kupanga Uzazi. Na ifahamike tu kwamba swala la kupanga uzazi lisiwe la Mwanamke peke yake,Uzazi bora huhusisha watu wawili yaani Mume na Mke katika Familia.
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUPANGA UZAZI NI PAMOJA NA;
1. Muda sahihi wa kupata watoto, hapa tunazungumzia umri(Interval) kati ya mtoto na mtoto, Wataalam wa afya wanashauri umri sahihi wa kupata watoto ambao ni mzuri kiafya uwe kuanzia miaka 2 au 3 kati ya mtoto na mtoto.
Hii huwapata watoto nafasi ya kupata muda wa kutosha wa kunyonya,Lishe N.K,hivo watoto huwa na afya bora zaidi na kuwa na Kinga ya kutosha dhidi ya Magonjwa mbali mbali ambayo huwasumbua sana watoto hasa wenye umri wa chini ya Miaka 5.
2. Kuzingatia sana katika kuchagua Njia sahihi kwenu,ambayo haitawaletea madhara au kuwasababisha mkapata watoto mapema au mkachelewa sana.
Mfano; Njia kama kalenda sio sahihi sana Kwa mtu ambaye Mzunguko wake unabadilika badilika yaani kwa kitaalam tunaita IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE hivo huweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kupata Mimba bila yeye kupanga.
Lakini pia Njia ya Uzazi wa Mpango aina ya Sindano,Huweza kuchelewesha sana Mwanamke kubeba mimba pale atakapohitaji kubeba,Hivo kusababisha mwanamke kukaa mda mrefu sana bila kupata Mtoto.
3. Kuzingatia kanuni za unyonyeshaji bora kwa watoto wote, ikiwemo ile ya kutowachanganyia watoto chakula na maziwa kabla ya kumaliza miezi 6, Mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama peke yake bila kuchanganyiwa na kitu kingine chochote kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzoni yaani kwa kitaalam hujulikana kama EXCLUSIVE BREASTFEEDING.
Na unyonyeshaji bora ni ule ambao unaenda hadi mtoto afikishe miaka miwili au mitatu ukiweza,huku akiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama pamoja na kuchanganyiwa na vitu vigingine baada ya miez sita ya mwanzoni.
4. Shirika la Afya Duniani yaani WHO linashauri idadi ya watoto katika familia liwe hadi Watano,ili kuhakikisha afya bora kwao, lakini na kwa Mama Pia.
KUMBUKA; Vitu vingine ambavyo ni vya muhimu vya kuzingatia katika kupanga uzazi ni pamoja na;
- Kuendelea kujitunza na kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na magonjwa mengine mbali mbali ambayo huweza kuwa hatari kwa wazazi wote wawili pamoja na mtoto aliye tumboni. Mfano wa magonjwa hatari ni kama; UKIMWI,KASWENDE pamoja na KISONONO.
- Kuendelea kudumisha hali ya usafi wa mwili pamoja na Mazingira ili kutokukaribisha magonjwa kama vile; Malaria,UTI,FANGASI,PID N.K ambayo yote haya huweza kuwa hatari kubwa kipindi cha Ujauzito.
- Kuepuka matumizi ya dawa hovio bila kufata maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!