AFYA TIPS
• • • • •
AFYA BORA KWA MTOTO HUJUMUISHA VITU GANI?(soma hapa kujua)
Tunapozungumzia mtoto kuwa na afya bora tunazungumzia vitu vyote ambavyo ni muhim kwa afya ya mtoto huyu.
Afya bora kwa mtoto ni pamoja na mtoto kutokuumwa umwa magonjwa, kupata usingizi mzuri,kuwa na kinga ya kutosha ya mwili N.K. Hebu tuangalie vitu ambavyo hujenga afya bora kwa mtoto
MSINGI WA AFYA BORA KWA MTOTO NI PAMOJA NA;
- mtoto kupata lishe nzuri,bora na ya kutosha, mfano; kama mtoto ni wa kunyonya maziwa ya mama pekee, hakikisha ananyonya vizuri kama inavyotakiwa, na kama ni wakula chakula hakikisha anakula chakula chnye virutubisho vyote muhimu mwilini.
- Hakikisha mtoto anakuwa safi muda wote, kwani usafi wa mwili kwa mtoto ni mojawapo ya nguzo imara ya afya bora na kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali kwa mtoto.
- Mahudhurio ya kliniki ya mtoto pamoja na mtoto kupimwa uzito ni muhimu sana katika kujua maendeleo na ukuaji wake.
- Hakikisha mtoto anapata chanzo zote anazotakiwa kupewa kuanzia anapozaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mutano.
NB; hivo basi hivi vitu vinne huweza kuwa dira na kuonyesha muelekeo wa kupata afya bora kwa mtoto wako, ambapo kwa ujumla wake nimetaja ;
1. Lishe bora kwa mtoto
2. Usafi wa mwili
3. Mahudhurio ya kliniki
4. Kupata chanzo zote muhimu
-
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!