AFYA NDYO MTAJI WAKO WA KWANZA(Je wajua hilo?)

 AFYA

• • • • •

AFYA NDYO MTAJI WAKO WA KWANZA(Je wajua hilo?)


Wengine wanasema kuwa na pesa ndyo mtaji wako wa kwanza. Lakini mimi nakuambia kwamba,Mtaji wako wa kwanza ni afya. Ukiwa unaumwa sana hata kama unapesa kiasi gani huwezi kufanya chochote.


Hebu fikiria unapesa nyingi alafu huna hata mtu mmoja wa kuzitumia au wa kukusaidia upo peke yako, Je pesa itakutoa kitandani au itaenda yenyewe ifanye kazi?


Ipende afya yako, na ipe kipao mbele cha kwanza kabla ya pesa. Maana yangu sio kwamba usitafte pesa,Lahasha! Pesa ni muhimu ila afya ni muhimu zaidi. Ili ufurahie pesa ulizo nazo lazima uwe na afya bora,ukiwa unaumwa hata kama unapesa huwezi kuzifurahia.


Jitahidi kufanya checkup za mara kwa mara na kwenda hosptal pale unapohisi dalili za ugonjwa wowote. Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume sio wepesi kwenda hosptal kuliko wanawake. 


Mwanamke akiumwa hupenda kwenda hosptal mara moja ili kujua afya yake pamoja na kupata matibabu. Mwanaume mpaka aume kiasi kwamba hawezi chochote ndyo anatafta hosptal. Huenda hii pia ikachangia vifo vingi vya akina baba katika familia na kuacha wake zao.


Fanya utafiti mdogo hata eneo ambalo limekuzunguka,utagundua katika familia nyingi wazazi wa kiume ndyo hutangulia kufa kabla ya Wanawake.


Je wewe unaipenda afya yako? au unapenda pesa kwanza?




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!