AFYA YA MAZINGIRA NA UMUHIMU WAKE KWAKO(je wajua mazingira yako yakiwa machafu huweza kukuletea magonjwa?)

 AFYA TIPS

• • • •

AFYA YA MAZINGIRA NA UMUHIMU WAKE KWAKO(je wajua mazingira yako yakiwa machafu huweza kukuletea magonjwa?)


Kuna watu wengi wanahangaika na afya zao pamoja na kwenda kujitibu magonjwa kila siku hosptal bila kufaham kwamba magonjwa wanayatoa katika mazingira waliopo. 


Afya ya mazingira ndyo hutengeneza afya yako pia. Afya ya mazingira ni pamoja na kuhakikisha mazingira yako yanakuwa safi na salama.  


Afya ya mazingira ni pamoja na kuhakikisha hukati miti kwenye vyanzo vya maji,na maeneo mengine, unahakikisha maji yanakuwa safi na salama, unafanya usafi kama kufagia na kukata maji marefu pamoja na kuondoa vichaka sehemu unapoishi N.K


UMUHIMU WA KUDUMISHA AFYA YA MAZINGIRA YAKO NI PAMOJA NA;


- Kukukinga na magonjwa mbali mbali ya Mlipuko kama vile Kipindupindu


- Kukuepusha na magonjwa kama Malaria ambayo hutokana na mbu kuzaliana maeneo ya vichaka pamoja na sehemu ambazo maji hutuama.


- Kukuepusha na ajali mbali mbali kama kung'atwa na wadudu,au wanyama wakali ikiwa ni pamoja na Nyoka,Nge N.K


- Kukuepusha kukatwa na vitu vyenye ncha kali kama chupa,pin, Nyembe,sindano N.K


- kukusaidia kupata hewa safi na salama


- Kukukinga na ugonjwa wa homa ya matumbo au typhoid ambao wengi huupata baada ya kunywa maji machafu


- Kukukinga na magonjwa mengine kama ya kuharisha,kutapika N.K



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!