AFYA YA MIGUU YAKO(nukuu ya leo)

 AFYA TIPS

• • • • • • 

AFYA YA MIGUU YAKO(nukuu ya leo)


Katika maisha ya binadamu miguu ni kiungo muhimu sana ambacho pia huhitaji matunzo pamoja na uangalizi wa karibu sana.


MAMBO YAKUZINGATIA KATIKA KULETA AFYA BORA YA MIGUU


1. Epuka kuvaa viatu ambavyo vina unyevu unyevu, kwani hutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi wa miguuni


2. Epuka kuvaa soksi ambazo hazijakauka vizuri, kwani hutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi wa miguuni


3. Epuka kutembea peku bila kuvaa kitu chochote miguuni kwani unajiweka kwenye hatari ya kupata madhara mbali mbali kama vile; majereha,kuchoma au kukatwa na vitu vya ncha kali, kuingiwa na minyoo aina ya hookworms N.K


4. Usafi wa miguu pamoja na mwili wote kwa ujumla wake ni muhimu kila siku


5. Hakikisha hauachi kucha ndefu za miguuni kwani huweza kuwa chanzo kizuri cha kubeba uchafu pamoja na vimelea vya magonjwa mbali mbali kama vile bacteria, Fangasi N.K


-


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!