Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANZO CHA MWANAMKE KUENDELEA KUPATA DALILI ZOTE ZA MIMBA WAKATI IMEHARIBIKA(hata akipima na UPT inaonyesha ipo)



 UJAUZITO

• • • •

CHANZO CHA MWANAMKE KUENDELEA KUPATA DALILI ZOTE ZA MIMBA WAKATI IMEHARIBIKA(hata akipima na UPT inaonyesha ipo)


Shida hii huwatokea wanawake wengi na wengine bila kuelewa shida ni nini au wafanyeje. 


Ukweli ni kwamba hatua ya kubeba mimba  huhusisha maandalizi mbali mbali ambayo hufanyika kwenye mwili wa mhusika.


Na moja ya vitu vikubwa ambavyo hutokea katika kipindi hiki ni mabadiliko ya vichocheo vya mwili, huku baadhi ya vichocheo vikizalishwa kwa wingi na vingine kupunguzwa sana.


Vichocheo kama progesterone na estrogen huzalishwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki,na husababisha mabadiliko mengi katika mwili wa mwanamke.


Kuna kichocheo kinachojulikana kama human chorionic gonadotrophin hormone(hcg) ambacho huzalishwa na placenta siku kadhaa kisha kuwepo kwenye mkojo,hiki ndyo hutumika kuonyesha mwanamke ni mjamzito kwa njia ya kipimo cha mkojo maarufu kama urinary pregnancy test au UPT.


Hivo basi  mabadiliko ya vichocheo vyote hivi kwa ujumla wake,ndyo husababisha mwanamke kupata dalili mbali mbali za mimba kama matiti kujaa,kutema mate sana,kupata kiungulia, kuhisi kichefuchefu,kutapika N.K


Kwahyo hata baada ya ujauzito kutoka, baadhi ya wanawake huendelea kupata dalili zote za mimba ikiwemo pamoja na kupima na kuona kabsa ujauzito upo kitu ambacho kinawachanganya wanawake wengi, kwani vichocheo hivi havirudi kwenye hali yake ya mwanzoni gafla au kwa siku moja, kuna mchakato au ni process. 


Hivo inakubidi ufaham kwamba unaweza ukapima kipimo kikasoma una mimba na wala mimba hauna. 


Ni muhimu kufanya vipimo vingine vikubwa kama Ultrasound N.K  ili kuhakikisha hali iliyopo ndani. 



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments