KIUNGULIA
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUPATWA NA KIUNGULIA(Au kwa kitaalam heartburn)
Tatizo hili huwapata watu wengi, wakiwemo wakina mama wajawazito. Zipo sababu kadhaa ambazo huchangia mtu kupatwa na hali ya kiungulia,na miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na;
- Kwa mama mjamzito, Mabadiliko ya vichocheo mwilini ambayo hutokea kipindi cha mimba,ndyo husababisha hali ya kiungulia. Hapa nazumgumzia vichocheo vya Progestrone pamoja na Relaxin
(i). Uzalishwaji mkubwa wa Kichocheo cha Progestrone kwenye damu kipindi cha ujauzito husababisha chakula kitembee taratibu pamoja na mmeng'enyo wake kwenda taratibu sana.
(ii). Uzalishwaji mkubwa wa kichocheo cha Relaxin kwenye damu kipindi cha ujauzito husababisha njia ya chakula yaani Oesophagus kutanuka, pamoja ma vichikizoo vya tumbo kulegea yaani Sphinter hali ambayo hupelekea chakula kilichopo tumboni kilichochanganyika na Acid kupanda juu, Hali hii husababisha kiungulia kikali kwa mama mjamzito
- Kula kwa wingi vyakula vyenye acid kali kama Maharage,kula vyakula vya mafuta mengi, Nyanya N.K
- Kunywa pombe kupita kiasi
N.K
DALILI ZA KIUNGULIA NI PAMOJA NA;
- Kuhisi hali ya kuchomwa inayopanda kifuani
- Kuhisi ladha ya kitu kichungu Mdomoni
- Na mara chache maumivu wakati wa kumeza mate
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!