MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA
• • • • •
DALILI ZA HATARI KWA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA
DALILI ZA HATARI KWA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA NI PAMOJA NA;
1. Mama baada ya kujifungua kuvuja damu kupita kiasi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Postpartum hemorrhage au PPH Kwa kifupi. Hali hii huweza kutokea ndani ya masaa 24 baada ya mama kujifungua yaani PRIMARY PPH au ndani ya kipindi cha wiki 6 za mwanzoni baada ya mama kujifungua au SECONDARY PPH
2. Mama baada ya kujifungua kupandisha homa mara kwa mara au joto la mwili kuwa juu
3. Mama baada ya kujifungua kupatwa na miwasho mikali sehemu za siri
4. Mkojo wa mama baada ya kujifungua kuanza kutoka wenyewe pasipo kujizuia, hii ni dalili ya tatizo la Fistula
5. Mama baada ya kujifungua kuona marue rue pamoja na kizunguzungu kikali
6. Mama baada ya kujifungua kuumwa na kichwa sana
7. Mama baada ya kujifungua kuanza tena kuvimba miguu
8. Mama baada ya kujifungua kupata maumivu makali ya tumbo juu kidogo ya kitovu au kwa kitaalam hujulikana kama Epigastric pain
9. Mama baada ya kujifungua kuanza kuhisi maumivu ya mgongo,kiuno pamoja na mkojo kuchoma wakati wa kukojoa
10. Mama baada ya kujifungua kuwa na hali kama ya kutetemeshwa mwili.
@ Kwa ushauri zaidi,elimu au tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584
UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII JAPO KWA UFUPI;
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!