DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA(Ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hypotension)
PRESHA YA KUSHUKA
• • • • •
DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA(Ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hypotension)
Kwa asilimia kubwa na kwenye makala nyingi za afya,watu huzungumzia kuhusu ugonjwa wa Presha ya kupanda. Japo kuna Presha ya kushuka, na huenda ukawa hufahamu kabsa dalili za Ugonjwa wa Presha ya kushuka ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hypotension.
Presha ya kawaida ni kuanzia 90-140 mmhg ya juu pamoja na 60-90 mmhg ya chini, Mfano; Ukiwa na presha ya 100/70mmhg presha yako ni nzuri na ni ya kawaida.
Presha ya kushuka,maana yake tunazungumzia presha ndogo kuliko wastani wa kawaida. Mfano; ukiwa na Presha ya 70/50mmhg presha yako iko chini kuliko kawaida.
DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kutokwa na jasho sana
- Mgonjwa kupata shida ya kuona au uoni hafifu
- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
- Mgonjwa kupata shida au tatizo la upumuaji
- Mgonjwa kupata hali ya kizunguzungu na wakati mwingine huweza kudondoka kabsa
- Mgonjwa kupoteza kumbukumbu, fahamu au kuchanganyikiwa
- Mgonjwa kuhisi baridi kali kwenye mwili wake
- Mgonjwa kuchoka kupita kiasi
- Mgonjwa kupoteza hamu ya chakula
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!