FAHAMU KUHUSU WATOTO MAPACHA(Maswali na majibu kuhusu watoto mapacha au Twins)

 WATOTO

• • • • •

FAHAMU KUHUSU WATOTO MAPACHA(Maswali na majibu kuhusu watoto mapacha au Twins)


SWALI 1: Hivi watoto mapacha unaweza kuwagundua kabla ya kujifungua?


MAJIBU; Ndyo,zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kugundua kama una mimba ya mapacha kama vile;


- Size au ukubwa wa tumbo


- Kwa kusikiliza mapigo ya moyo ya watoto


- Kwa kutumia kipimo cha ultrasound


SWALI 2: Hivi watoto mapacha huweza kupatika kutoka kwa mwanaume mmoja?


MAJIBU; Ndyo, kuna aina mbili za mapacha kama ifuatavyo;


- Mapacha wanaofanana; ambao hupatika kwa njia ya mbegu moja ya mwanaume kulirutubisha yai na baada ya urutubishaji yai moja likagawanyika mara mbili na kutoka watoto wawili.


- Mapacha wasio fanana; ambao huwa ni mbegu mbili ambazo hufanikiwa kuingia kwa mayai mawili tofauti na baada ya urutubishaji tunapata watoto wawili.

   Kwa hapa sasa,mbegu hizo huweza kutoka kwa mwanaume mmoja au wanaume wawili tofauti.


SWALI 3: Eti mapacha wanaweza kuzaliwa huku wameshikana?


MAJIBU; Ndyo, katika hali isiyo ya kawaida ya kiuumbaji,watoto hawa wawili huweza kuzaliwa wakiwa wameungana.


SWALI 4: Watoto mapacha wanaweza kuzaliwa kwa wakati mmoja au mmoja hzaliwa saiv na mwingine kukaa baada ya siku au mwezi?


MAJIBU; Watoto mapacha huweza kuzaliwa wote kwa wakati mmoja wakati mama anajifungua,mmoja akatangulia na baada ya muda kidogo mama akapata uchungu tena akajifungua wapili.


SWALI 5: Watoto mapacha huweza kufanana kila kitu?


MAJIBU; ndyo hasa hasa aina ya kwanza ambayo nimeiyelezea ya mapacha wanaofanana au kwa kitaalam hujulikana kama Identical twins. Mapacha hawa huweza kufanana vitu vingi mpaka kundi lao la damu kuwa sawa.


KWA MASWALI ZAIDI,ELIMU AU USHAURI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Kama unapenda watoto weka COMMENT hapa..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!