DIALYSIS
• • • • •
FAHAMU KWA KINA HUDUMA YA KUSAFISHA DAMU MAARUFU KAMA DIALYSIS
Huduma hii hutolewa kwa watu ambao wana matatizo ya Figo kama vile; Figo kufeli na kushindwa Kufanya kazi. Ambapo wataalam wa afya hushauri huduma hii kuanza endapo Uwezo wa figo kufanya kazi utapotea kwa zaidi ya asilimia 85-90% pamoja na uwepo za kuchuja yaani Glomerular filtration rate(GFR) kuwa chini ya <15.
Utaanza kujiuliza maswali,je sasa huduma ya kusafishwa damu au Dialysis ina uhusiano gani na kumsaidia mgonjwa wa Figo kufeli? Majibu yapo hapa chini;
HUDUMA YA KUSAFISHWA DAMU AU DIALYSIS HUFANYA MAMBO YAFUATAYO;
Baada ya figo zako kufeli na kushindwa kufanya kazi yake, huduma ya kusafisha figo huuweka mwili katika hali ya kawaida au Body balance state kwa;
1. Kuondoa uchafu wote mwilini(waste products), Chumvi chumvi pamoja na kuzuia maji kukusanyika mwilini.
2. Kuhakikisha baadhi ya kemikali muhimu sana mwilini zinakuwa katika kiwango salama kwenye Damu,Mfano; potassium, Sodium pamoja na bicarbonate.
3. Pia huduma ya kusafisha damu au Dialysis husaidia sana katika kudhibiti kiwango cha Presha kwenye Mwili wa Mgonjwa.
JE HUDUMA HII YA KUSAFISHWA DAMU AU DIALYSIS HUTOLEWA KWA MUDA GANI?
• Endapo mgonjwa ana matatizo ya Figo kushindwa kufanya kazi kwa muda fupi yaani Acute kidney failure, Huduma hii ya kusafishwa damu huweza kufanyika mpaka pale uwezo wa figo utakapoimarika na kurudi katika hali yake ya kawaida.
• Lakini endapo tatizo la figo kushindwa kufanya kazi ni la kudumu yaani Chronic Kidney failure basi huduma hii ya kusafishwa damu au Dialysis hutolewa katika kipindi cha maisha yako yote.
KUMBUKA; Moja ya vitu vya kuzingatia kwa mtu mwenye matatizo ya figo kufeli au kushindwa kufanya kazi ni pamoja na kuzingatia Ulaji wake wa kila siku na kuacha kabsa matumizi ya pombe.
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!