Ticker

6/recent/ticker-posts

FANGASI WA KWENYE DAMU,DALILI ZAKE,VIPIMO NA MATIBABU YAKE



 FANGASI

• • • • • •

FANGASI WA KWENYE DAMU,DALILI ZAKE,VIPIMO NA MATIBABU YAKE


Kuna aina nyingi za mashambulizi ya fangasi huku mashambulizi hayo yakihusisha maeneo mbali mbali katika mwili wa binadamu. Mfano;


~ Kuna fangasi wa kwenye Damu(ambao ndyo tunazungumzia katika makala hii)


~ kuna fangasi wa kwenye Ulimi


~ Kuna Fangasi wa mdomoni


~ Kuna fangasi wa tumboni


~ Kuna fangasi wa miguuni


~ Kuna fangasi wa sehemu za siri Mfano ukeni 


~ Kuna fangasi wa kooni


N.K


FANGASI WA KWENYE DAMU

-  Haya ni maambukizi ya Fangasi ambayo hutokea kwenye Damu ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Systemic Mycoses, na mwanzo kabsa hutumia Njia ya mapafu kabla ya kuingia kwenye Damu na kuleta madhara mbali mbali.


DALILI  ZA UWEPO WA FANGASI WA KWENYE DAMU NI PAMOJA NA;


1. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kichwa


2. Mgonjwa kupata uchovu kupita kiasi pamoja na mwili kukosa nguvu


3. Mgonjwa kupata maumivu makali eneo la kifuani


4. Joto la mwili kupanda au Mgonjwa kupata homa za mara kwa mara


5. Mgonjwa kupatwa na hali ya mwili kutetemeka


6. Mgonjwa kupata shida katika kupumua


7. Mgonjwa kupata maumivu makali ya misuli,joint pamoja na Mifupa ya mwili


8. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kikohozi cha mara kwa mara


9. Uzito wa mwili kwa Mgonjwa kupungua kwa kiasi kikubwa


10. Mgonjwa kuhisi maumivu wakati wa kutembea, hivo kupelekea hata wengine kutembea kwa shida au kushindwa kabsa kutembea.


11. Pia kuna wakati Mgonjwa huweza kupata athari kwenye Ngozi kama vile,ngozi kuwasha sana,kubadilika rangi na kuwa nyekundu N.K


VIPIMO VYA FANGASI WA KWENYE DAMU


- Fangasi wa kwenye damu huhusisha vipimo mbali mbali kama vile; vya kuchukua Sample ya damu kutoka kwa Mgonjwa na kuchunguzwa maabara, Kutumia Hadubini N.K


- Kutumia kipimo cha antigen test ambacho huhusisha mkojo wa Mgonjwa au Damu yake


- Kupima makohozi ya mgonjwa mwenye dalili za Fangasi wa kwenye Damu


- Kupima na kuchunguza maji ya uti wa Mgongo kutoka kwa Mgonjwa

N.K


MATIBABU YA FANGASI WA KWENYE DAMU 


• Matibabu ya aina hii ya fangasi huhusisha matumizi mbali mbali ya Dawa za Fangasi kama vile; Echinocandin, Dermofulvin au Griseofulvin, Itraconazole, Ketoconazole N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







Post a Comment

0 Comments