POMBE
• • • • • •
HANGOVER YA POMBE(Chanzo cha Hali ya uchovu)
Sababu kubwa ya mtu kupatwa na hali hii ni kutokana na kupoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini au kwa kitaalam tunaita Dehydration kwani pombe ni mojawapo ya Diuretics na husababisha mwili wako upoteze maji kwa wingi kwa njia mbali mbali kama vile; kukojoa sana mara kwa mara, Hivo kupelekea wewe kupatwa na madhara mbali mbali kama vile;
- Uchovu wa mwili kupita kiasi
- Hali ya kuwa na kizunguzungu kikali
- Kupatwa na maumivu makali ya kichwa
Nb; Watafiti wa afya husema pombe ambazo ni za rangi au zenye rangi huchangia kwa kiwango kikubwa tatizo hili la mtu kuwa na hangover baada ya kunywa pombe kutokana na kuwepo kwa kemikali aina ya Congeners ambazo husababisha hali ya kutekenya(irritate) mishapa ya damu pamoja na tisu za ubongo wako.
TAHADHARI KWA MNYWAJI WA POMBE
- Usinywe pombe na carbonated soda. Soda huongeza speed ya pombe kuingia kwenye damu
- Usinywe pombe tumbo likiwa tupu. Kabla ya kunywa hakikisha umekula, chakula hupunguza kiwango cha pombe kinachoingia kwenye damu
- Usinywe pombe kwa pupa, ini lina uwezo wa kuchakata gram 8 za pombe kwa saa, Sawa na bia moja kwa saa
(đź“ťNormanJonasMD)
#afyabongo #drtareeq
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!