IJUE HOMA YA UTI WA MGONGO(MENINGITIS) CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE

HOMA YA UTI WA MGONGO

• • • • • •

IJUE HOMA YA UTI WA MGONGO(MENINGITIS) CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE


Homa ya uti wa mgongo ni tatizo ambalo huweza kutokea kwa mtu yeyote bila kujali umri au jinsia. Homa hii ya uti wa Mgongo huweza kutokea baada ya mashambulizi ya eneo la Uti wa Mgongo pamoja na ubongo. Mashambukizi haya huweza kuwa ya Fangasi,Virusi au Bacteria.


CHANZO CHA TATIZO LA HOMA YA UTI WA MGONGO


- Homa ya uti wa mgongo husababishwa na mashambulizi ya aina mbali mbali za virusi,bacteria pamoja na Fangasi, Kama ifuatavyo;



1. Kuna mashambulizi ya Fangasi kama vile; Cryptococci meningetides.


2. Kuna mashambulizi ya bacteria kama vile; Neisseria Meningitides,Escheria coli na Listeria Monocytogenes


3. Kuna mashambulizi ya virusi kama vile; Herpes Simplex


DALILI ZA TATIZO LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kuwa na tatizo la mwili kutetemeka au kutingishwa ambapo kwa kitaalam tunaita fits


- Mgonjwa kuwa na hali ya kukakamaa kwa misuli yake ya mwili


- Mgonjwa kuwa na tatizo au shida ya kukakamaa shingo na kuwa ngumu hata kugeuka


- Mgonjwa kuwa na tatizo la kuumwa na kichwa sana


- Joto la mwili kwa mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kupandisha homa


- Endapo tatizo hili litatokea kwa mtoto mdogo,utosi wake huweza kuvimba


- Mgonjwa kuwa na shida ya kupoteza fahamu zake


N.K


MATIBABU YA TATIZO LA HOMA YA UTI WA MGONGO


Matibabu ya tatizo la homa ya uti wa mgongo hutegemea sana na chanzo chake husika,Mfano; Kama mgonjwa ana shida ya homa ya Uti wa Mgongo kutokana na mashambulizi ya bacteria,basi bacteria hao huzibitiwa kwa dawa mbali mbali kama vile Cefriaxone au Powersafe kama wengine walivyozoea, 


Kama shida ya homa ya uti wa mgongo ni kutokana na mashumbulizi ya virusi,basi virusi hao huzibithiwa kwa dawa mbali mbali kama vile Acyclovir


Kama shida ya homa ya uti wa mgongo ni kutokana na mashumbulizi ya fangasi,basi fangasi hao huzibithiwa kwa dawa mbali mbali kama vile flucytosine N.K


KUMBUKA; Epuka matumizi ya dawa hovio pasipo maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya,Kwani dawa isipotumiwa kwa usahihi wake huweza kugeuka na kuwa Sumu,badala kutibu basi ikaua.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!