HOMA
• • • •
JE HOMA NI UGONJWA AU NI NINI?(soma makala hii)
Katika hali ya kawaida watu wengi wakipata homa, wanasema ninaumwa ugonjwa wa homa, ila kimsingi homa sio ugonjwa,bali homa ni dalili za ugonjwa flani.
Moja ya viashiria vinavyotolewa na mwili wako kuhusu magonjwa mbali mbali ambayo yameshambulia mwili wako ni pamoja na joto la mwili kupata au kuwa na homa.
Hivo basi katika mapambano kati ya kinga yako ya mwili na vimelea vya magonjwa ambavyo vimeshambulia mwili wako kama vile bacteria na virusi mbali mbali, husababisha hali ya joto la mwili kupanda yaani kuwa na homa
Hivo homa ni kiashiria na dalili kwamba ndani ya mwili wako kuna shida au kuna mashambulizi ya vimelea flani ambavyo sio rafiki na salama kwa afya yako
MASHAMBULIZI YA MAGONJWA AMBAYO HUWEZA KUSABABISHA JOTO LA MWILI KUPANDA AU HOMA NI PAMOJA NA
1. kuwa na ugonjwa wa UTI au maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo
2. Kupatwa na ugonjwa wa malale maarufu kama Trypanosoma
3. Kupatwa na mashambukizi ya virusi vya UKIMWI
4. Kupatwa na mashambulizi ya virusi vya Corona
5. Kuumwa ugonjwa wa Malaria
6. Kupatwa na ugonjwa wa PID au maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke
7. Kupatwa na maambukizi kwenye mapafu
8. Kuumwa na ugonjwa wa homa ya ini
9. Kuumwa na magonjwa mbali mbali ya moyo
10. Kuumwa na ugonjwa wa homa ya Uti wa mgongo
11. Kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi wa kwenye damu na maeneo mengine
12. Aina mbali mbali za kansa au saratani kama vile; saratani ya mapafu, saratani ya matiti,saratani ya shingo ya kizazi N.K
-
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!