JE KUHARISHA NI TATIZO?(Soma makala hii..!!)

 KUHARISHA

• • • • •

JE KUHARISHA NI TATIZO?


Hali hii ya kutoa kinyesi cha maji maji huweza kutokea kwa kila mtu, Wa jinsia yoyote(mwanaume au mwanamke),wa umri wowote(mtoto,kijana na hata mzee).


Kama tulivyozoea kwamba endapo mtu akiharisha basi huenda ni dalili ya Ugonjwa flani ambao umempata kama vile ugonjwa wa homa ya matumbo kwa kitaalam typhoid,Ugonjwa wa Malaria N.K.


Lakini leo nikungue macho uelewe hii; Sio kila wakati ukiharisha basi ni vibaya,Lahasha! wakati mwingine ni faida kubwa kwako kiafya.


Mwili una tabia ya kupambana na kila aina ya kitu kigeni ambacho kinaingia kwenye mwili wako, Hapa nitatolea mfano; Endapo umekula chakula lakini chenye uchafu mwingine,mwili wako huweza kukupa taarifa kwa kuanza kuonyesha reaction mbali mbali kama vile tumbo kuuma na mwisho wa siku kuhakikisha huo uchafu ambao umeingia kwa njia ya kula chakula unatoka nje ya mwili wako kwani haukufai. 


Basi moja ya njia ambayo hutumika ni kutoa uchafu huo kwa kujisaidia  haja kubwa. Hapo ndipo mtu huanza kupata maumivu ya tumbo pamoja na kuharisha.



KWA USHAURI ZAIDI KUHUSU AFYA YAKO,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!