MIMBA
• • • •
JE KUKOJOA NJE HUWEZA KUKUKINGA USIPATE MIMBA?(njia ya uzazi wa mpango)
Kuna watu wengi hutumia njia hii ya kukojoa nje wakati wa tendo la ndoa na kuamini kwamba inaweza kuwa njia ya uzazi wa mpango ya wao kuitumia.
Je njia hii ina usahihi kwa asilimia mia moja 100%, Na je inawezekana kutumia njia hii? Hatari yake ni nini?
Katika hali ya kawaida ni kwamba ili mwanamke asipate mimba au urutubishaji usitokee basi lazima yai la mwanamke lisikutane na mbegu ya mwanaume.
Hivo basi chochote utakachofanya ambacho kitazuia mbegu ya mwanaume isikutane na yai la mwanamke utakuwa umefanikiwa kuzuia mimba kwa asilimia 100%.
Ukweli ni kwamba swala la mwanaume kukojoa nje wakati anafanya mapenzi na mwanamke ili mwanamke asipate mimba ni swala ambalo huhitaji umakini na utulivu wa hali ya juu.
MADHARA YA KUTEGEMEA NJIA HII KAMA NJIA YA KUPANGA UZAZI
- Ni njia ambayo huhitaji umakini wa hali ya juu
- Ni rahisi sana mwanamke kubeba mimba hasa pale akili ya mwanaume ikijisahau
- Njia hii huweza kuathiriwa na vitu kama vile; msongo wa mawazo kwa mwanaume, hasira,furaha sana,hamu sana,utamu sana N.K
vitu ambavyo huweza kupelekea mwanaume kushindwa na kupoteza uwezo wa kujizidhibiti wakati wa kufanya tendo la ndoa, Kitu ambacho hupelekea mbegu za mwanaume kuingia ndani na mwanamke akapata mimba.
- Haina uhakika wa asilimia mia moja 100%, huathiriwa na vitu kama hisia za mtu,mazingira N.K
Muhimu sana kuongea na wataalam wa afya ili kukushauri njia salama kwako.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!