JE KUUMWA NA TUMBO SANA WAKATI WA HEDHI NI KAWAIDA?(soma kujua)

 HEDHI

• • • • • 

JE KUUMWA NA TUMBO SANA WAKATI WA HEDHI NI KAWAIDA?(soma kujua)


Wanawake wengi hupata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, japo kuna vitu unatakiwa kuvijua ili uweze kutofautisha maumivu ya kawaida na maumivu ambayo huashiria mwanamke ana tatizo lingine.


MAUMIVU YA TUMBO AMBAYO SIO YA KAWAIDA WAKATI WA HEDHI


- Endapo unapata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi hadi kufikia hatua ya kulazwa hospital, ujue huenda una tatizo lingine kama vile; maambukizi katika via vyako vya uzazi au PID N.K


- Endapo unapata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi ambayo huambatana na Joto la mwili kupanda yaani HOMA, huenda ukawa na shida nyingine kama vile UTI


- Endapo unapata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi huku yakiambatana na kukosa pumzi pamoja na uchovu wa mwili kupita kiasi, hii sio hali ya kawaida nenda hosptal kwa ajili ya uchunguzi zaidi


- Endapo unapata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi huku yakiambatana na kutapika sana, haya sio maumivu ya kawaida,nenda hosptal kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi


N.K


Hivo ni baadhi tu ya viashiria ambayo nimevitaja kukuonyesha uweze kutofautisha maumivu ya tumbo wakati wa hedhi  ambayo ni ya kawaida na ambayo sio ya kawaida.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!