JE MAMA MWENYE MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI ANAWEZA KUZAA WATOTO AMBAO HAWANA?
VIRUSI VYA UKIMWI PAMOJA NA UKIMWI WENYEWE(HIV/AIDS)
• • • • •
JE MAMA MWENYE MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI ANAWEZA KUZAA WATOTO AMBAO HAWANA?
🔻 INAWEZEKANA.! NAFIKRI WALE AMBAO WANANIULIZA SANA HILI SWALI MMEPATA MAJIBU KWA KUSOMA MAKALA HII;
Mama ambaye tayari ana maambukizi ya virusi vya ukimwi yaani VVU, Licha ya kuwa na tatizo la UKIMWI lakini anaweza kuzaa watoto ambao hawana maambukizi kabsa na pia anaweza kuishi na mwanaume ambaye hana maambukizi kabsa na asimwambukize. Hili linawezekana vipi?
Endapo mama ana maambukizi ya virusi vya ukimwi na anatumia dawa kwa usahihi kabsa pamoja na kufwatilia/kuzingatia kwa makini maelekezo anayopewa na wataalam wa afya katika nyanja hii, anaweza kabsa kuwa na familia Bora isiyo na maambukizi yoyote ya Virusi vya ukimwi.
FAHAMU HILI; Endapo mama atatumia dawa za ARV's kwa usahihi kabsa na kwa kufata mashariti yote ya Dawa kutoka kwa wataalam wa afya,atasababisha Wingi wa Virusi vya ukimwi kushuka chini yaani kwa kitaalam tunaita Low Viral Load, pamoja na hali ya kufubaza Kabsa Virusi vya ukimwi(VVU) hivo kusababisha Virusi vya Ukimwi kukosa Nguvu ya kuambukiza mtu.
KWA KUONGEZEA TU NJIA AMBAZO HUWEZA KUKUHATARISHA WEWE KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI NI PAMOJA NA;
- Kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama nyembe,sindano,Pin N.K
- Kufanya ngono zembe yaani kufanya mapenzi bila kinga au Kondom
- Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
- Kuwa na wapenzi wengi
- Kuchangiwa damu ya mtu mwenye Virusi vya ukimwi
ILA MTU HAWEZI KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA;
- Kushikana mikono na muathirika wa ukimwi
- Kukaa pamoja na muathirika wa ukimwi
- Kwa kushare vyombo vya kula kama sahani,vijiko N.K
- Kwa kukumbatiana na mtu mwenye Virusi vya ukimwi
- Kwa kung'atwa na Mbu.
KUMBUKA; Kuna maisha baada ya kuambukizwa Virusi vya ukimwi,hivo bado dunia inakuhitaji wewe na bado dunia inakutegemea wewe amka sasa.
•
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUNAWEZA KUWASILIANA KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!