JE NI MUDA GANI MTOTO HUANZA KUCHEZA TUMBONI? NA ASIPOCHEZA INA MAANA GANI?
MTOTO
• • • • •
JE NI MUDA GANI MTOTO HUANZA KUCHEZA TUMBONI? NA ASIPOCHEZA INA MAANA GANI?
Kwa kawaida Mtoto kucheza tumboni huanzia ujauzito ukiwa na kipindi cha wiki 20-24.
Wakina mama wengi wajawazito huanza kumsikia mtoto akicheza katika kipindi hiki cha wiki 20 mpaka 24, na asilimia kubwa ya akina mama wajawazito,mapigo ya moyo kwa mtoto huanza kusikika ujauzito ukiwa na kipindi cha Wiki 24.
Hivo basi hata wataalam wa afya huanza kutumia kipimo cha kusikiliza mapigo ya moyo kwa mtoto maarufu kama Fetolscope, Kama kwenye picha hapo chini, Mama akiwa na mimba yenye umri wa wiki 24.
ANGALIZO; Endapo mama, ujauzito wake umefikia umri wa mtoto kucheza, na huenda wengine walishaanza kumsikia mtoto akicheza tayari, basi kitendo hiki kinatakiwa kuwa endelevu. Hivo mtoto kuacha kucheza tumboni zaidi ya masaa 24 kwa wewe ambaye ujauzito wako umefikia umri wa mtoto kucheza tumboni,basi hilo ni tatizo.Nenda hospital haraka kwa ajili ya kupata msaada wa kiafya.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!