JE UMEPATWA NA TATIZO LA KUKOJOA USAHA?(fahamu chanzo cha tatizo hili)

 USAHA

• • • • •

JE UMEPATWA NA TATIZO LA KUKOJOA USAHA?(fahamu chanzo cha tatizo hili)


Tatizo hili la kukojoa usaha huwatokea sana wanaume zaidi ya wanawake, japo hata wanawake pia huweza kupatwa na shida hii. Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuwa chanzo kikubwa cha wewe kukojoa usaha kama vile;


- Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya Zinaa kama vile Kisonono au kwa kitaalam tunaita Gonorrhea.


- Kupatwa na tatizo la tezi Dume( kwa wanaume pekee)


- Maambukizi mengine ambayo huhusisha mfumo wa Mkojo kama UTI


- Kupatwa na uvimbe kwenye Njia ya mkojo


- Kuota kijibu kwenye njia ya mkojo na kupasuka kwa ndani


- Kupatwa na sumu kali kama vile 4-aminodephly,pia huweza kusababisha wewe kupatwa na shida ya kukojoa usaha


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa


- Kupatwa na maumivu makali wakati wa kukojoa


- Kupatwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu


- Mkojo kuchoma wakati wa kukojoa


- Kutokwa na usaha.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!