JINSI YA KUJISAFISHA UKIWA CHOONI(afya kwa mwanamke)

 CHOONI

• • • • •

JINSI YA KUJISAFISHA UKIWA CHOONI(afya kwa mwanamke)


Katika hali ya kawaida watu hujisafisha kwa mazoea kama walivyofundishwa wakiwa wadogo na wengine wanasema kama walivyozoea, ila kuna jinsi ya kujisafisha na kuepuka kupatwa na magonjwa.


Hii ni maalumu kwa wanawake,kwani ndyo wahanga wakubwa wa tatizo hili, Na wengine hupatwa na magonjwa mbali mbali kama UTI bila wao kujua chanzo husika ni kipi.


• Kutokana na maumbile ya mwanamke yalivyo, mwanamke hushauriwa zaidi kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma na sio kutoka nyuma kwenda mbele baada ya kujisaidia chooni.


• Hii ni kwa sababu endapo mwanamke atajisafisha kutoka nyuma kwenda mbele, yupo kwenye hatari ya kutoa uchafu kutoka kwa haja kubwa na kuingiza sehemu zake za siri


Hali ambayo humuweka mwanamke katika hatari ya kupatwa na magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa huu wa UTI(urinary track infection au maambukizi katika mfumo mzima wa mkojo).


Hivo basi jenga mazoea na tabia ya kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma na sio kutoka nyuma kwenda mbele, kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.


Hii itakusaidia sana kukukinga na magonjwa kama UTI ambayo hutokea mara kwa mara hasa kwa wanawake zaidi ya wanaume.


-


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!