MIMBA
• • • • • •
JINSI YA KUJUA UMRI WA MIMBA(Maalumu kwa mama mjamzito)
Moja ya vitu muhimu sana kwa mama mjamzito ni kujua umri wa mimba au ujauzito aliobeba. Wakina mama wengi hawana elimu ya kutosha hasa kwa wale ambao ndyo mimba zao za kwanza hivo hupata shida sana katika kipindi hiki.
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUJUA UMRI WA MIMBA YAKO
Kitu cha muhumu kwako kuliko vyote ni kukumbuka tarehe ya kwanza ya hedhi ya mwisho kwa kitaalam Hujulikana kama First day of Last normal menstrual period (LNMP). Hapa namaanisha hivi;
Unatakiwa kujua hedhi yako ya mwisho ilikuwa tarehe gani, Mfano; tarehe 1/02/2021 ndipo hedhi yako ya mwisho kabla ya kugundulika kwamba una mimba ilianza. Au kwa maneno mengine baada ya hii hedhi kuisha hukupata hedhi nyingine mpaka kugundulika kwamba ni mjamzito.
Baada ya hapo ilichukua siku ngapi,Mfano; ilichukua siku tatu kuanzia tarehe 1,2 na 3.
Sasa basi siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho itakuwa ni tarehe 1. Kwa ufafanuzi huu nafikiri utakuwa umenielewa. Hapo ndipo mahesabu ya kukusaidia Kujua tarehe yako ya matarajio ya kujifungua huanza.
Wanawake wengi wajawazito wanakisia tarehe hizi hivo husababisha kupata majibu ambayo sio sahihi kuhusu umri wa mimba,hata wengine kufikia hatua ya kuona tarehe za matarajio ya kujifungua(Expected date of delivery (EDD)) zimepita sana, kumbe sio.
MAELEKEZO NA MAHESABU YA JINSI KUTUMIA TAREHE YA HEDHI KUJUA TAREHE SAHIHI YA MATARAJIO YA KUJIFUNGUA
Kwanza Zingatia haya;
(i). Tunajumlisha 7 kwenye sehemu ya tarehe
(ii). Tunamjumlisha 9 kwenye mwezi, kuanzia mwezi 3 kushuka chini, yaani mwezi wa 3,2 na 1. Halafu mwaka unabaki vile vile au jumlisha 0.
(iii). Tunatoa 3 kwenye mwezi, kuanzia kwezi wa nne na kuendelea. Halafu tunajumlisha 1 kwenye Mwaka.
MFANO;
1. Tarehe ya kwanza ya hedhi ya mwisho; 1/02/2021
- Tarehe 1 / 02 / 2021
+ 7 / + 09 / + 0
JUMLA 8/ 11/ 2021
Hivo Tarehe ya matarajio ya kujifungua ni TAREHE 8/11/2021.
2. Tarehe 1/04/2021
- Tarehe 1 / 04 / 2021
+ 7/ - 3 / +1
JUMLA 8/ 01/ 2022
Hivo Tarehe ya matarajio ya kujifungua ni TAREHE 8/01/2022.
HIVO BASI KUJUA UMRI WA MIMBA KUNA NJIA KUU NNE AMBAZO NI;
1. Kwa kutumia Mahesabu
2. Kwa kutumia kipimo cha Ultrasound
3. Kwa kutumia kikokotoo cha mimba maarufu kama Pregnancy Wheel
4. Na Kwa kutumia tape measure
INAENDELEA...!!!!
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!