JINSI YA KUONDOKANA NA MSONGO WA MAWAZO(njia sahihi)

 MSONGO WA MAWAZO

• • • • •

JINSI YA KUONDOKANA NA MSONGO WA MAWAZO(njia sahihi)


Kila mtu katika maisha yake kwa namna moja au nyingine huweza kupitia kipindi hiki kigumu cha kuwa na msongo wa mawazo au kwa kitaalam tunaita Severe depression.


Hali hii huweza kuchangiwa au kusababishwa na sababu mbali mbali kama vile; changamoto ya kiuchumi, changamoto ya kimahusiano,Familia, Elimu, Ndoa, Uzazi N.K


DALILI ZA MTU MWENYE MSONGO WA MAWAZO NI PAMOJA NA;


- Mtu kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu bila kumaliza, wakati ni kitu kidogo tu cha kufanya dakika mbili


- Mtu kuanza kuongea mwenyewe


- Mtu kuongea vitu ambavyo haviwezekaniki katika hali ya kawaida


- Mama kuanza kuongea habari za kumuua mtoto ambaye kamzaa mwenyewe au mama kuanza kuongea habari za kujiua mwenyewe

N.K



JINSI YA KUONDOKANA NA MSONGO WA MAWAZO(njia sahihi)


- Epuka hali ya kujitenga na kukaa mwenyewe kila mara,Jichanganye na watu mbali mbali ambao wanaweza kukufanya usiwe na mawazo

- Kama ulikua husali,jitahidi kwenda Ibada kanisani au Msikitini. Tafiti zinaonyesha kwamba,Moja ya Njia kuu za kumsaidia mtu mwenye msongo wa mawazo kuondokana na hali hii, ni kusali, 


Watu wengi ambao hujihusisha na mambo ya Mungu Hujenga Msuli wa Imani ambao utawafanya hata kama wamekata tama,wainuke tena na kujiona kiumbe kipya.


- Fanya mazoezi ya mwili,moja ya vitu ambavyo humfanya mtu kuondokana na Stress au Msongo wa mawazo ni kujishuhulisha na kufanya mazoezi ya mwili kila siku, Hivo mbali na faida zingine za mazoezi kiafya mwilini, pia humsaidia mtu kuondokana na msongo wa mawazo.


- Jishuhulishe na michezo mbali mbali unayoipenda kama vile Kucheza Mpira wa Miguu, Mpira wa kikapu,Kuruka kamba N.K


- Sikiliza muziki unaoupenda au angalia Movies mbali mbali kama wewe ni mpenzi wa Movies au Series.

N.K


Kama bado tatizo lipo kutana na Wataalam mbali mbali wakiwemo, wataalam wa afya na Wataalam wa Saikolojia Kwa ajili ya matibabu zaidi.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!