KIPI KINAWEZA KUWA CHANZO KIKUBWA KWA MWANAMKE MJAMZITO KUJIFUNGUA KWA NJIA YA UPASUAJI?
UPASUAJI
• • • • • •
KIPI KINAWEZA KUWA CHANZO KIKUBWA KWA MWANAMKE MJAMZITO KUJIFUNGUA KWA NJIA YA UPASUAJI?
Katika hali na harakati za mtoto kuzaliwa,zipo njia kuu mbili tu ambazo mtoto huweza kuzaliwa Njia hizo ni; Kuzaliwa kwa Njia ya kawaida yaani kwa kitaalam tunaita Spontenous Vagina Delivery au mtoto Kuzaliwa kwa Njia ya upasuaji na njia hii kwa kitaalam hujulikana kama Ceasarian Section(C/S).
Wapo wakina mama wengi siku hizi ambao hujifungua kwa Njia hii ya upasuaji,huku shida hii ikichangiwa na sababu mbali mbali
SABABU ZA MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA KWA NJIA YA UPASUAJI NI PAMOJA NA;
1. Mama mjamzito kuwa na Njia ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa mtoto,hivo mtoto kushindwa kupita na kuzaliwa kwa Njia ya kawaida,hali hii kwa kitaalam tunaita Cephalopelvic Disproportion. Ambapo njia kuwa ndogo huweza kuchangiwa na vitu mbali mbali ikiwemo; Mfupa wa Nyonga kubana yaani kwa kitaalam tunaita Contracted Pelvis, au mwanamke kuwa na mfupa wa nyonga aina ya kiume ambapo tunasema Male Pelvis type
2. Sababu nyingine ni mtoto kuwa mkubwa sana ambapo hali hii kwa kitaalam hujulikana kama Big baby. Hivo basi hata kama Njia ya mama ipo kawaida kwa mtoto kupita,Lakini kwa mtoto ambaye ni mkubwa yaani Big baby hawezi kupita kabsa.Hivo itamlazimu mama huyu kufanyiwa upasuaji au kujifungua kwa Njia ya Upasuaji.
3. Mama kuishiwa nguvu ya kusukuma mtoto mbali na jitahada za wataalam wa afya, shida hii huweza kumpelekea mama mjamzito kufanyiwa upasuaji ili kumuokoa yeye pamoja na mtoto aliyetumboni.
4. Mama kupatwa na Kifafa cha Mimba,Tatizo hili pia huweza kuchangia mama mjamzto kufanyiwa upasuaji au kujifungua kwa Njia ya Upasuaji.
5. Sababu nyingine ni mama mjamzito kupatwa na tatizo la Kondo la nyuma kushuka na kujishikiza sehemu ya chini katika mji wa mimba na kupelekea kuziba kwa Mlango wa uzazi ambapo mtoto anatakiwa kupita,hali hii kwa kitaalam hujulikana kama Placenta praevia.
6. Mama mjamzito kupatwa na shida ya Kondo la nyuma kuachia kabsa sehemu ambapo lilikuwa limejishikiza hivo kupelekea hali ya mtoto kuwa hatarini na mama pia,Tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Placenta abruption na huweza kuchangia mama kujifungua kwa Njia ya upasuaji.
7. Mtoto kupatwa na shida tumboni ikiwemo pamoja na mapigo ya moyo kubadilika yaani Fetal Distress, hali ambayo huhitaji msaada wa haraka kwa mama huyu.
8. Sababu nyingine ni mwanamke kuomba mwenyewe kwa ridhaa yake kwamba anahitaji kufanyiwa upasuaji kwa sababu anazozijua yeye; ikiwemo ile ya kusema eti Kujifungua kawaida kuna uchungu zaidi, au eti kunaharibu reception(yaani sehemu zake za siri).
9. Mwanamke kufanyiwa upasuaji katika mimba za nyuma,japo haimaanishi kila mwanamke ambaye ujauzito uliopita kajifungua kwa upasuaji lazima na ujazito huu ajifungue kwa njia hii ya upasuaji,lahasha! inategemea na sababu ya kufanyiwa upasuaji ni nini.
10. Mwanamke kupatwa na tatizo la kuanza kublid wakati mimba imekaribia kujifungua,hali hii pia huweza kuchangia wataalam wa afya kumfanyia upasuaji mama huyu baada ya uchunguzi wa kina.
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
TAZAMA VIDEO HII;
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!