Ticker

6/recent/ticker-posts

KULALA VIBAYA HUWEZA KUKULETEA BAADHI YA MADHARA KIAFYA(soma hapa)



 KULALA

• • • • •

KULALA VIBAYA HUWEZA KUKULETEA BAADHI YA MADHARA KIAFYA(soma hapa)


Kuna baadhi ya watu husema leo nimelala vibaya kila sehemu kunauma. 


Ukweli ni kwamba kuna jinsi unatakiwa ulale ili kuepuka kupata madhara mbali mbali kama vile;


- Tatizo la kuumwa sana na mgongo


- Tatizo la kuumwa na shingo


- Tatizo la kuumwa na kiuno


- Tatzo la kuumwa na miguu


- Tatizo la kuumwa sana na kichwa


- Tatizo la kuumwa na tumbo


- Kuota ndoto nyingi wakati wa usiku


N.K


Katika hali ya kawaida,wataalam wa afya hushauri mtu kupendelea kulala ubavu wa kulia au kushoto ili kuruhusu mzunguko mzuri wa damu hasa hasa kutoka kwenye mshipa mkubwa wa damu unaopita sehemu ya nyuma mgongoni maarufu kama Inferior vena cava.


Ushauri huu huenda mbali zaidi kwa mama mjamzito huku akisisitizwa kulalia zaidi upande wake kwa kushoto au ubavu wake wa kushoto ili kuepuka kugandamiza mshipa huu na kupata madhara mbali mbali kama vile;


• Kushuka kwa shinikizo la damu yaani hypotension


• Maji kujaa sehemu ya chini ya mwili kama miguuni, na miguu kuvimba


• Matatizo kama ya kukosa hewa yakutosha kwa mtoto na mama pia


• Mapigo ya moyo kwenda mbio zaidi


Hivo kulala kifudifudi(kulalia mgongo), kulalia tumbo,yote hii milalo sio mizuri kwa afya yako katika hali ya kawaida.



KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments