KUUMWA WAKATI UKIWA SAFARANI NI UGONJWA GANI? (Fahamu kuhusu Motion Sickness)
SAFARINI/KUUMWA
• • • • • •
KUUMWA WAKATI UKIWA SAFARANI NI UGONJWA GANI? (Fahamu kuhusu Motion Sickness)
Kuna baadhi ya watu wakisafiri huwa wagonjwa kabsa, na baada ya safari au baada ya kufika wanapoenda huwa wazima kabsa, kwa maana nyingine ugonjwa wao hutokea wakati wakiwa safarini tu. Je ushawahi kufikiria hili ni tatizo gani? na je ni hali ya kawaida au shida ni nini?.
Huu ni ugonjwa kama magonjwa mengine, na ugonjwa huu kwa kitaalam hujulikana kama Motion Sickness ambapo Mtu mwenye ugonjwa huu hupatwa na matatizo mbali mbali akiwa safarini.
DALILI ZA UGONJWA HUU WA KUUMWA UKIWA SAFARINI AU MOTION SICKNESS NI PAMOJA NA;
-Tumbo kuuma sana
- Mvurugiko wa tumbo
-kuharisha
- kuwa na shida ya mate kujaa mdomoni
- Kukosa hamu ya kula chakula
- Kusikia kichefu chefu na kutapika sana
- Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa ya mpauko au Pale skin
-Kupatwa na hofu kubwa au woga
- Kupatwa na kizunguzungu
Kuwa na hali ya kutoa jasho hata kama hamna joto
- Wengine kufikia hatua ya kupoteza kabsa fahamu
- Kuumwa na kichwa sana
- Kupata shida ya kuvuta na kutoa hewa au kuwa na shallow breath kwa kitaalam.
- Kuwa na uchovu wa mwili kupita kiasi
N.K.
CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUUMWA WAKATI WA SAFARINI(MOTION SICKNESS)
Ugonjwa huu wa motion sickness hutokana na kupingana na kutofautiana kwa milango ya fahamu kwenye Mfumo wa fahamu ndani ya mwili wako pindi ukiwa safarini, Mfano;Macho yako huona kitu kingine,misuli yako ya mwili huhisi kitu kingine, na masikio yako ya Ndani huhisi kitu kingine(Kwa ufupi hakuna ushirikiano).
Mvurugiko huu wa taarifa ambazo hazina ushirikiano ukifika kwenye ubongo,ubongo wako hushindwa kutafsiri,hivo kukupelekea kuanza kupata madhara tu kama vile; kizungu zungu,kichefuchefu,kutapika, jasho,woga, na wakati mwingine kwa baadhi ya watu hupoteza kabsa fahamu.
NINI CHA KUFANYA IKITOKEA UPO SAFARINI,UMEPATWA NA UGONJWA HUU WA MOTION SICKNESS?
1. Changanya Ndimu au Limao pamoja na Asali alafu tumia.
2. Matumizi ya tangawizi husaidia pia kwa kiasi kikubwa kwani hufanya kazi kubwa ya ufyonzwaji wa acid mwilini.
3. Kama upo kwenye gari lala na egemeza kichwa chako kwenye siti ya gari ili kuleta hali ya utulivu katika sehemu ya ndani ya sikio lako.
4. Epuka matumizi ya pombe ukiwa safarini
5. Pia unaweza kufanya kazoezi kadogo tu ka kuvuta masikio yako kuelekea kwa chini,kitendo hiki husaidia kuongeza mzunguko katika sehemu ya ndani ya sikio lako na kukusaidia kuondoa hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika.
6. Matumizi ya pipi aina ya Ivory,nina imani wengi wanazifahamu,husaidia pia kuondoa hali ya kichefuchefu na kutapika ukiwa safarini.
7. Upe ubongo wako mda wa kurelax, na kutokujihusisha na vitu kama vile; kusoma vitabu,N.K
8. Pia unaweza kutumia dawa kama vile; vitamin B complex kidonge kimoja pamoja na magnessium kidonge kimoja ili kuzuia hali ya kichefuchefu.
9. Jaribu kuangalia sehemu moja kwa mda kidogo,sio kila upande na kila sehemu hasa ukiwa umekaa sehemu ya dirishani mwa gari ambapo ni pazuri zaidi kwani pia utapata hewa ya kutosha.
10. Unaweza kusikiliza nyimbo unazozipenda na za utulivu ili kuufanya ubongo wako urelax.
11. Lakini pia tafiti zinaonyesha kwamba, watu wenye tatizo hili la kuumwa wakiwa safarini au Motion sickness,wakisafiri wakati wa Usku hali hii hutulia kabsa.Hivo unaweza kusafiri usku pia,kama inawezekana.
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!