KWANINI WATU HUPATWA NA NJAA KALI BAADA YA KUNYWA POMBE?

POMBE

• • • • • •

KWANINI WATU HUPATWA NA NJAA KALI BAADA YA KUNYWA POMBE?


Ni jambo linalowakumba wengi mno haswa wanapomaliza kupata 'mbili tatu' na wengine hata hushangaa Kwani walikuwa wamekula na kushiba vizuri kabla ya kunywa pombe. Ama baada ya kunywa mtu anaporudi nyumbani akafakamia vilivyopo kama ni mkate uliobaki ama chochote akikutacho lakini kesho yake asubuhi 'Hangover' inakuja na njaa kali kama si yeye aliyefakamia vyakula masaa machache yaliyopita. Zifahamu sababu kuu 3 


1. Iko hivi, Pombe huwa na tabia ya kuchezea kiwango cha sukari kwenye damu kwa kuutaarifu ubongo kuwa una njaa hivyo ule zaidi. Hii hutokea kwa pombe kuamsha 'signals' za ubongo zihusikazo na njaa. Kimombo tunaweza iweka hivi, 'alcohol activates the brain signals that tell the body to eat more food' na hii hutokea mara nyingine hata ukiwa huna njaa. Lakini pia, kunywa pombe kunaweza kupunguza Kiwango cha sukari kwenye damu kwa muda tu(temporarily) hivyo, baada ya kunywa mwili wako unajaribu kukuarifu kuwa una njaa ili glucose mwilini ipatikane


2. Jambo jingine ni, Kupungukiwa maji mwilini (dehydration). Pombe ni diuretic kama vile zilivyo dawa kama Lasix, hivyo humfanya mtu akojoe zaidi. Na unapokojoa zaidi ndivyo unavyopoteza zaidi maji mwilini na kama hu 'replace' maji hayo utaanza kuhisi kiu. Na hapa ndipo kwenye shida, watu huchanganya kiu na njaa, badala ya kunywa maji, hufakamia chakula zaidi na zaidi


3. Pia, kuna swala la mwili wako kufanya kazi ya ziada kujitahidi kuiondoa pombe kwenye system. Tunapokuwa tumelala, protini hutengenezwa ili kulisaidia ini kuondoa vitu ambavyo miili yetu huchukulia ni sumu (toxins) katika damu. Hivyo mwili huchoma calories ili kuiondoa pombe ilhali wakati huohuo ini halitengenezi nguvu ya kutosha kwa sehemu nyingine za mwili. Hivyo unapoamka tu na Hangover ya pombe, mwili hukuambia ule ili ufidie nguvu ilotumika


NINI CHA KUFANYA?

Unapohisi njaa baada ya kunywa, ni vizuri ukala lakini usifakamie haswa vyakula visivyofaa 'junky foods'. Kwa kuwa kunywa pombe hupunguza uwezo wa mwili kufyonza virutubisho baadhi kama vitamin B12, thiamine na folate, basi ni vyema kula mayai, cheese, maharagwe na karanga. Pia, kunywa maji ya kutosha


Ama hakikisha unakula mlo wa asubuhi wenye virutubisho muhimu 


Via drtareeq




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!