MABADILIKO YA MWILI KATIKA UKUAJI WA MTOTO(balehe)

 BALEHE

• • • • •

MABADILIKO YA MWILI KATIKA UKUAJI WA MTOTO(balehe)


Desturi ya wazazi kuongea na watoto wao kuhusu mabadiliko mbali mbali ambayo huwatokea watoto katika miili yao kipindi cha ukuaji wao bado ni changamoto.


Lakini kuna umuhimu mkubwa wa watoto kujifunza na kujua mabadiliko hayo ili kuweza kujiandaa na kujikinga ili wasiingie sehemu mbaya, sio swala la kufundishwa shuleni tu na waalam hata mzazi pia ni jukumu lake.


YAJUE BAADHI YA MABADILIKO YA MWILI KIPINDI CHA UKUAJI WA MTOTO(BALEHE)


- Kuanza kuwa na chunusi za usoni kwa wanawake na wanaume


- Nywele kuota maeneo ya siri pamoja na kwapani kwa wanawake na wanaume


- Sauti ya kike kuwa nyororo zaidi tofauti na mwanaume


- Sauti ya kiume kuwa nzito na besi tofauti na mwanamke


- Umbo la mwili kuanza kubadilika na kuchukua sura ya kiutu uzima ikiwemo na kuwepo kwa hips kwa mwanamke


- Kwa mwanaume kuanza kuota ndevu


- Katika kipindi hiki ndyo tabia nyingi huanza kujitokeza maana ni kipindi tunasema cha try and error


- Wanaume na wanawake kuanza kujifunza kushiriki mapenzi kitu ambacho kimepelekea maambukizi mengi ya virusi vya ukimwi kutokea katika umri huu wa balehe


- Kuanza kujishirikisha na tabia hatarishi kama wizi uvutaji wa sigara,bangi,unywaji wa pombe pamoja na madawa mengine ya kulevya


- Watoto kuanza kuwa watukutu hata kwa watu walio wazidi umri


- Hiki ndyo kipindi ambacho mtoto hutaka kujifunza na kujaribu kila kitu


- Kwa mwanamke kuanza kupata hedhi yake ya kwanza na mayai yake kukomaa hivo kuwa katika hatari ya kupata mimba


- Kwa mwanaume kuanza kutoa mbegu za kiume au kwa lugha nyingine kumwaga shahawa hivo kuwa katika hatari ya kumbebesha mwanamke mimba


- Kuanza kuota matiti na kutuna ambapo kwa mwanamke huwa makubwa zaidi ya mwanaume


- Ngozi ya mwili hasa kwa mwanamke kuwa nyororo zaidi kuliko hapo mwanzo


- Hamu ya kufanya mapenzi kuongezeka sana


N.K


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!