POMBE
• • • • •
MADHARA YA POMBE KWENYE MWILI WAKO
Ushawah kuskia huu msemo kwamba "Pombe si Chai" Na ni kweli pombe sio chai kwani ina madhara makubwa katika mwili wa mtumiaji. Tafiti zinaonyesha kwamba madhara ya kunywa pombe ni mengi kuliko faida zake katika mwili wa Mtumiaji.
MADHARA YA POMBE KWENYE MWILI WAKO NI PAMOJA NA;
1. Kuathiri utendaji kazi wa Ini na kuharibu kabsa Ini, Ini ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu, na ni miongoni mwa viungo ambavyo hufanya kazi nyingi sana katika mwili wako. Moja ya kazi kubwa ya ini ni kupambana na kila aina ya sumu inayopitishwa kwenye mwili wako ambapo tunasema ini linafanya mchakato mzima au process ya Detoxification. Sasa unywaji wa pombe husababisha ini kushindwa kufanya kazi vizuri ikiwa ni pamoja na kupelekea hali ya seli hai za ini kufa na kuleta tatizo linalojulikana kama Cirrhosis.
2. Matatizo ya Figo, Moja ya shida kubwa inayowapata walevi wa pombe ni Kufeli kwa Figo au tatizo la Figo kushindwa kufanya kazi, Ambapo huchangiwa na kuathiriwa kwa mfumo mzima wa damu ikiwa ni pamoja na kusukuma damu kutokana na kunywa Pombe.
3. Matatizo ya Presha,hii hutokana na ukweli kwamba unywaji wa pombe hubadilisha na kuathiri mfumo mzima wa mzunguko wa damu mwilini, hivo kupelekea mtumiaji kuwa na matatizo mbali mbali ikiwemo hili la Presha au shinikizo la Damu.
4. Magonjwa ya Moyo, Baada ya pombe kuathiri mfumo mzima wa kusukuma damu, Basi na matatizo mengine huweza kutokea kama vile mishipa ya moyo kushindwa kusukuma damu vizuri ndani ya moyo na kupelekea mtu kuwa na shida ya damu kuganda au hata moyo wenyewe kuwa na matatizo.
5. Kupatwa na magonjwa mbali mbali hasa ya Zinaa, Kumbuka miongoni mwa watu wanaongoza kwa kufanya ngono zembe ni walevi wa pombe, Hivo kuwaweka katika hatari ya kupata magonjwa mbali mbali kama vile; Chlamydia,Kisonono,kaswende, au Ukimwi.
6. Kuathiri utendaji kazi wa Seli nyekundu za damu au Red blood cells
7. Kuwa katika hatari ya kupatwa na Magonjwa kama Kisukari
8. Kuwa katika hatari ya kupata shida ya Uzito kuwa mkubwa au kupita kiasi
9. Kuwa katika hatari ya Kupata tatizo la Saratani au Kansa, Hii ni kutokana na kwamba unywaji wa pombe husababisha mwili kuingia katika mchakato mzima wa kubadilisha kilevi yaani ALCOHOL kwenye pombe kuwa katika Mfumo wa Acetaldehyde.
10. Unywaji wa pombe huweza kuathiri eneo la Ubongo na kumfanya mnywaji kuwa mtu wa kupoteza kumbukumbu pamoja na fahamu kwa wakati mwingine.
11. Pombe huweza kuathiri mfumo mzima wa uzazi ikiwa ni pamoja na uwezo wa mwanaume kuzalisha mbegu za kiume za kutosha ambapo tatizo hili hujulikana kama Low Sperm count,hivo mwanaume kupoteza uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
12. Unywaji wa pombe ni chanzo kikubwa cha mtu kuwa na shida ya Gauti,ndyo maana Mgonjwa wa Gauti anashauriwa kuacha pombe kabsa.
13. Pombe huweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto aliyetumboni kipindi mama mjamzito akinywa pombe, na madhara hayo huweza kuhusisha uumbaji wa mtoto(ulemavu), shida ya ubongo pamoja na matatizo ya uti wa Mgongo.
14. Unywaji wa pombe huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa Kwa Mwanaume kuwa na tatizo la Kukosa Nguvu za kiume.
KUMBUKA; "Pombe Sio Chai" See you next session.
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!