MAJI
• • • • •
MAJI NI UHAI(Nukuu ya leo)
Bila shaka usemo huu sio mgeni kwenye masikio yako, kwamba maji ni uhai, tukiwa na maana kwamba bila maji hakuna maisha.
Maji hutumika kwenye kila hatua ya maisha ya binadamu, kama kwenye kupikia,kuogea,kufulia,kuwanyeshea mifugo wako, kunywa N.K
Ni dhahiri kwamba bila maji hakuna kinachoendelea kwenye maisha ya binadamu.
Wataalam wa afya wameenda mbali zaidi na kuthihirisha kwamba zaidi ya asilimia 75% ya mwili wa binadamu ni maji. Hivo maji ni uhai
UMUHIMU WA MAJI MWILINI NI MKUBWA SANA
- Maji ndyo husaidia katika mfumo mzima wa umeng'enyaji chakula mwilini
- Maji ndyo husaidia katika kutoa taka mwili nje ya mwili kwa njia ya kukojoa
- Maji ndyo husaidia katika kuleta afya ya seli hai za mwili
- Maji ndyo husaidia katika Kuleta uhai wa kila kiungo cha mwili wako ikiwa ni pamoja na afya ya bongo,figo N.K
- Maji ndyo husaidia wewe kupata choo kwa raha na sio kigumu wala kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
- Maji ndyo husaidia kukukinga na magonjwa mbali mbali kama yale ya mfumo mzima wa mkojo mfano; UTI
KUMBUKA; Tafiti zinaonyesha mtu anayekunywa maji kwa wastani wa lita 2.5 kwa siku hupunguza uwezakano wa kuugua ugonjwa wa UTI za mara kwa mara kwa zaidi ya asilimia 50%
Tunashauriwa tunywe maji angalau kuanzia lita 2.5 mpaka 3 kwa siku au ndani ya masaa 24 ili kuweza kupata afya bora ya miili yetu.
Kumbuka "Maji ni Uhai"
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!