UZAZI
• • • • •
MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA FANYA YAFUATAYO(muhimu kwa afya yako)
Haya ni baadhi ya mambo muhimu sana kwa mama baada ya kujifungua, hivo kama wewe upo kwenye kundi hili, makala hii ni ya muhimu sana kwako.
1. Hakikisha usafi wa mwili wako muda wote,kinga dhidi ya magonjwa
2. Lishe bora bila kusahau vitu vya kuongeza damu kwani damu nyingi hupotea wakati wa kujifungua
3.Tenga muda kwa ajili ya mazoezi na muda kwa ajili ya kupumzika
4. Hakikisha unaenda kliniki baada ya siku 7, siku 28 na siku 42. Watu wengi hawajui kwamba kuna kliniki kwa mama baada ya kujifungua na wengi hawahudhurii.
5. Anza kutumia njia ya uzazi wa mpango ambayo ni sahihi kwa mwili wako,ili upate mtoto mwingine baada ya miaka 2 au 3
6. Jikinge na magonjwa mbali mbali kama vile; Malaria na Ukimwi
7. Mnyonyeshe mtoto kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzoni bila kumchanganyia na kitu kingine chochote hata maji
8. Nenda haraka kituo cha afya ambacho kipo karibu na wewe ukihisi unaumwa wewe au mtoto
9. Usiweke kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto,wala usifunge kitovu na kitu kingine chochote
10. Mtoto asiogeshwe kwenye maji mengi mpaka kitovu chake kidondoke
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!