MARCH 22 LEO NI SIKU YA MAJI DUNIANI(Tuangalie ugonjwa wa kuharisha kwa watoto)

SIKU YA MAJI DUNIANI

• • • • • •

MARCH 22 LEO NI SIKU YA MAJI DUNIANI(Tuangalie ugonjwa wa kuharisha kwa watoto)


SABABU ZA za KUHARISHA KWA WATOTO 


Kuharisha kunaweza kusababishwa na aina mbalimbali za vimelea ingawa pia kunaweza kusitokane na maambukizi ya vimelea (non-infectious causes). Vimelea vinavyosababisha kuharisha ni


1. Virusi: Virusi vinaongoza katika kusababisha tatizo la kuharisha kwa watoto katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Kuna aina takribani 4 wanaojulikana ambavyo ni Rotavirus, Adenovirus, astrovirus na norovirus. Kati ya hivi jamii ya Rotavirus ndio wanaongoza duniani kote katika kueneza na kusababisha kuharisha kwa watoto wachanga na wadogo . Katika nchi zinazoendelea, Rotavirus ndiyo chanzo kikuu cha vifo vinavyotokana na kuhara miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka 5.


2. Bakteria: Wanasababisha kuharisha kwa asilimia chache 2-10%. Kuharisha kunakosababishwa na bacteria husababisha upotevu mdogo wa maji ukilinganishwa na virusi. Mfano wa bakteria wanaoweza kusababisha tatizo hili ni Campylobacter, Salmonella, Shigella, na Escherichia coli


3. Parasite pia husababisha kuhara, lakini aina hii ya kuhara huwa ni sugu zaidi (chronic diarrhea) kwa ujumla na mara nyingi haiambatani na homa, kutapika, na upungufu wa maji mwilini. Giardia lamblia na Cryptosporidium parvum ni moja ya aina hii za parasire wanaosababisha kuhara.


Sababu ambazo hazihusiani na maambukizi ya vimelea yaani noninfectious causes ni pamoja na kula chakula kilichochanganywa na sumu au kumeza sumu, matatizo katika sehemu ya utumbo mwembamba na mnene, na matatizo ya usagaji chakula (metabolic abnormalities).

. .


NAMNA YA KUZUIA MAAMBUKIZI 


1. Kuzingatia usafi wa chakula (kupika na kuhifadhi). .

.

2. Kunawa mikono kila baada ya kutoka chooni, kabla ya kushika chakula na wakati wa kula


3. Kuwa makini na watoto wanaoharisha ikiwezekana kuwatenga na wenzao


4. Matumizi ya Chanjo


Cc: drtareeq




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!